Na Coletta Wanjohi
Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa Tume ya Haki za Kibinadamu nchini Sudan Kusini. Tume hiyo iliundwa Machi 2016 na mamlaka yake imeongezwa kila mwaka tangu wakati huo.
Kazi yake inahusisha kufuatilia na kutoa ripoti kuhusu hali ya haki za binadamu Sudan Kusini.
"Kuvunja mtego wa kutokujali kunaweza tu kuafikiwa ikiwa mamlaka ya kitaifa itajitolea tena na kuzingatia thamani na ahadi katika mkataba wa amani," Barney Afako, mmoja wa makamishna watatu wa tume hiyo alisema katika taarifa.
2013 ghasia zilizuka Sudan Kusini kufuatia mapambano ya kisiasa kati ya rais Salva Kiir na makamu wake wa wakati huo Riek Machar. Mnamo 2018, pande zinazozozana zilitia saini makubaliano ya amani ili kumaliza mzozo huo.
Serikali ya mpito iliundwa mwaka 2020, ambayo jukumu yake ni pamoja na kuandaa uchaguzi.
Mnamo Agosti 2022, serikali hii ilitangaza kwamba muda wa mpito utaongezwa kwa miezi 24 zaidi. Muda huu ulifaa kumalizika mnamo 2023.
Je, Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu nchini Sudan Kusini inafanya nini?·
- Tume hili ni chombo huru, ambacho kinapokea mamlaka yake kutoka kwa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa.
- Linaongozwa na makamishna watatu wanaohudumu kwa uhuru
- kukusanya na kuhifadhi ushahidi wa ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu nchini Sudan Kusini
- kutoa mwongozo kuhusu haki na mchakato wa uwajibikaji na upatanisho nchini Sudan Kusini
- kushirikiana na serikali ya Sudan Kusini na mashirika mengine husika katika kukuza uwajibikaji kwa ukiukaji wa haki za binadamu.
·
·