Watu 45,000 walijisajili kwa mbio za Great Ethiopian Run mwaka huu / Picha kutoka Great Ethiopian Run

Kampuni ya Great Ethiopian Run inasema, zaidi ya wakimbiaji 45,000 walijisajili kushiriki katika mbio za Great Ethiopian Run, jijini Addis Ababa nchini Ethiopia. Mbio hizo zinavutia watu kutoka Ethiopia, Afrika na duniani kote.

Mwanariadha mashuhuri wa Ethiopia Haile Gebrselassie aliazisha hafla hiyo mwaka 2001/ picha kutoka ET

Mbio za mwaka huu ziliadhimisha miaka 23 ya hafla hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2001 na mwanariadha mashuhuri wa Ethiopia - Haile Gebrselassie ili kukuza kukimbia kama shughuli ya kiafya.

Maelfu ya watu huja kwa ajili ya furaha na michezo/ picha by Great Ethiopian Run

Kila mwaka idadi ya wanaohudhuria inaongezeka, wengi wakija kwa ajili ya kufurahia na familia na marafiki zao.

Medali hupewa kila mtu anayehusika katika mbio hizo/ picha kutoka Great Ethiopian Run

Watu wengine hukimbia na wengine kutembea tu lakini kila mtu hupata medali.

Great Ethiopian Run imekuwa ishara ya umoja kwa Waethiopia/ picha kutoka  Great Ethiopian Run

Mbio hizo ni zaidi ya mbio tu; ni sherehe ya utamaduni wa umoja wa Ethiopia. Imekuwa ikichangia sana katika kudumisha na kukuza amani na umoja miongoni mwa Waethiopia.

Watu wengi kutoka Afrika Mashariki pia walijumuika katika mbio za mwaka huu | picha:  Timothy Mlay        

Kila mwaka wanariadha wa kulipwa wenye ulemavu hukaribishwa kuhusika katika kitengo chao maalum za mbio hizo.

Wanariadha wenye ulemavu pia hujuishwa/  picha kutoka Great Ethiopian Run

TRT Afrika