Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan. Picha: AA

Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ameonya juu ya "njama kubwa" ya kusambaratisha umoja wa nchi hiyo.

"Sudan inalengwa kupitia njama kubwa ya kuiharibu na kudhoofisha umoja wake," Al-Burhan alisema alipokuwa akizungumza katika mkutano na maafisa polisi katika jimbo la mashariki la Bahari Nyekundu.

"Sudan inalengwa kupitia njama kubwa ya kuiharibu na kudhoofisha umoja wake," Al-Burhan alisema alipokuwa akizungumza katika mkutano na maafisa wa polisi katika jimbo la mashariki la Bahari Nyekundu.

Hata hivyo, Burhan hakutoa maelezo yoyote kuhusu madai ya njama hiyo.

Sudan imekumbwa na mzozo kati ya jeshi na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) tangu Aprili na kusababisha vifo vya raia 3,000 huku maelfu wakijeruhiwa katika vita hivyo, kulingana na matabibu wa eneo hilo.

"Vyombo vyote vya kawaida (vya usalama) vitajitahidi kukabiliana na njama hii na kuizuia," Al-Burhan alisema kwenye matamshi yake aliponukuliwa na taarifa iliyotolewa na Baraza la Utawala wa Mpito, Sudan.

Ameapa kuviwajibisha vikosi vya RSF kwa kushiriki uhalifu wa kivita katika mji mkuu Khartoum na jimbo la Darfur magharibi.

Makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano iliyosimamiwa na wapatanishi wa Saudia na Marekani kati ya wapinzani hao wanaozozana imeshindwa kumaliza ghasia nchini humo.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linakadiria kuwa karibu watu milioni nne wamekimbia makazi yao kutokana na mzozo wa sasa unaoendela nchini Sudan.

Kipindi cha mpito cha Sudan, kilichoanza Agosti 2019 baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais Omar al-Bashir, kilipangwa kumalizika na uchaguzi mapema 2024.

TRT Afrika na mashirika ya habari