Kumbukumbu ya maafa ya ukoloni yagubika ziara ya Mfalme Charles III nchini Kenya

Kumbukumbu ya maafa ya ukoloni yagubika ziara ya Mfalme Charles III nchini Kenya

Takriban watu 10,000 waliuawa wakati wa kukandamiza harakati za Mau Mau dhidi ya wakoloni wa Kiengereza.
Mamlaka ya kikoloni ya Uingereza iliweka hali ya hatari katika kukabiliana na uasi wa Mau Mau / Picha: AFP

Mfalme Charles III wa Uingereza anatarajiwa kuanza safari ya siku nne nchini Kenya kuanzia Oktoba tarehe 31 hadi Novemba 3.

Hii ni ziara yake ya kwanza kama mfalme katika taifa la Jumuiya ya Madola, ambapo maoni yoyote atakayotoa kuhusu historia ya ukoloni wa Uingereza yataangaliwa kwa karibu.

Charles anatarajiwa kukabiliana na "mambo machungu " ya uhusiano wa kihistoria wa Uingereza na Kenya, kasri ya Buckingham imesema.

Hiki ni kipindi cha ukoloni wa Uingereza nchini Kenya, uliokwisha mwaka wa 1963.

Hii itajumuisha "Dharura" ya 1952-1960, wakati mamlaka ya kikoloni ilipoweka hali ya hatari katika kukabiliana na kampeni ya msituni ya Mau Mau dhidi ya walowezi wa Ulaya.

"Mfalme atachukua muda katika ziara hiyo kuongeza uelewa wake wa makosa yaliyotendeka katika kipindi hiki kwa watu wa Kenya," Kasri ya Uingereza ilisema mapema mwezi huu, ikitangaza safari hiyo.

Hisia tofauti

Takriban watu 10,000 - hasa kutoka jamii ya kabila la Wakikuyu nchini Kenya - waliuawa wakati wa kupigania uhuru.

Huenda ziara ya kifalme ikapokelewa kwa hisia tofauti.

Safari ya mfalme huyo pia inajiri huku taifa hilo la Afrika likijiandaa kusherehekea miaka 60 ya uhuru kutoka kwa Uingereza mwezi Desemba.

Chaguo la Kenya katika ziara yake ya kwanza tangu awe mfalme mnamo Septemba lina uzito kwa familia ya kifalme.

Ilikuwa nchini Kenya mnamo 1952 ambapo mama yake Charles - marehemu Malkia Elizabeth II - alipata habari ya kifo cha baba yake, Mfalme George VI, kuashiria mwanzo wa utawala wake wa kihistoria wa miaka 70.

Charles na mkewe Malkia Camilla watakaribishwa na Rais wa Kenya William Ruto jijini Nairobi siku ya Jumanne.

Historia ya ukoloni

Lakini historia ya ukoloni haitakuwa mbali na ziara ya mfalme huyu.

Baada ya kesi mahakamani iliyodumu kwa miaka kadhaa, Uingereza ilikubali mwaka wa 2013 kuwafidia zaidi ya Wakenya 5,000 ambao waliteswa wakati wa Mau Mau.

Hii ilikuwa katika mkataba wa thamani ya karibu pauni milioni 20 (takriban dola milioni 25 kwa viwango vya kubadilisha fedha vya leo).

Baada ya Prince William kuonyesha "huzuni kubwa" kwa biashara ya utumwa wakati wa safari ya Jamaica mwaka jana, na kuacha kuomba msamaha rasmi, maneno ya Charles nchini Kenya "yataangaliwa kwa karibu sana," kulingana na mtaalam Cullen

" Ikiwa ataomba msamaha au anaonyesha majuto basi nchi zingine "zitatarajia kitu chenyewe". "Nadhani itaweka aina ya mfano," Cullen aliongeza.

Charles amefanya ziara tatu za awali rasmi nchini Kenya, mwaka 1971, 1978 na 1987, na mfalme na malkia pia wameitembelea nchi hiyo kwa faragha.

TRT Afrika