Mkenya Beatrice Chebet alinyakua dhahabu akifuatiwa na Faith Kipyegon na Sifa Hassan wa Uholanzi akachukua nafasi ya tatu/Picha: Reuters 

Sakata ya shindano la mbio za mita 5000 za wanawake katika mashindano ya olimpiki ya Paris 2024 yameishia kwa Faith Kipyegon wa Kenya kurejeshewa medali yake ya dhahabu.

Bingwa huyo wa dunia wa mbio za mita 1500 za wanawake, alijikuta katika msukumano na mkinzani wake matata wa Ethiopia Gudaf Tsegay wakati imesalia mizunguko miwili tu kumalizika.

Kipyegon alifahamishwa juu ya adhabu aliyopewa ya kumpokonya medali yake ya fedha alipokuwa akielekea kuzungumza na wanahabari katika sehemu yao waliyotengewa.

"Nimesikitishwa na kile ambacho kimetokea hivi punde, naambiwa nimepokonywa medali, sijui ni kwa nini…sijui kilichotokea," Kipyegon mwenye hisia kali alisema.

Aliongeza, “Kilichotokea kati yangu na Gudaf ni kwamba nilikuwa mbele na alikuwa anataka kunipita, lakini nilimwambia kuwa atanisukuma nje ya njia, lakini aliendelea kusukuma na kujiuliza nikimbilie wapi?"

Baada ya kisa hicho Kipyegon na kikosi cha Kenya waliwasilisha rufaa kwa kamati husika ya Olimpiki na dakika 30 baada ya kurejelea picha hizo, walimuondolea Kipyegon makosa na kumrejeshea medali yake.

Wanariadha wenzake wa timj ya Kenya, mabingwa wapya wa Olimpiki Chebet na Margaret Chelimo walisema Gudaf alistahili kuadhibiwa na wala sio Kipyegon kwani ndiye aliyemsukuma bingwa huyo wa Olimpiki mara mbili katika mbio za mita 1500.

Kipyegon alisema sasa anaangazia mbio za Jumanne za mita 1500 raundi ya 1 ambazo ni maalum kwake anapotafuta kushinda hat-trick ya medali za dhahabu katika mbio za raundi tatu na nusu.

Matokeo licha ya kukumbwa na kashfa yalipatia Kenya ushindi wa dhahabu na fedha wakiongozwa na Beatrice Chebet aliyevuka utepe kwa muda wa ushindi wa dakika 14, sekunde 28.56 (14:28.56).

Mholanzi mwenye asili ya Ethiopia Sifan Hassan alinyakua nafasi ya shaba kwenye medali kwa kumaliza nyuma ya Kipyegon kwa muda wa 14:30.61.

TRT Afrika