Ubalozi wa Kenya nchini Uingereza umewatahadharisha raia wake wanaoishi nchini humo kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo yanayotolewa na serikali ya nchi hiyo.
Kauli hii inafuatia maandamano yanayoendelea nchini humo yaliyoratibiwa na watu wa mrengo wa kulia dhidi ya wahamiaji na waislamu.
“Wakenya wanashauriwa kujisajili katika Ubalozi wa Kenya uliopo nchini Uingereza kupitia tovuti rasmi za Ubalozi,” imesema taarifa ya Ubalozi.
Kwa wiki kadhaa sasa, Uingereza imeshuhudia maandamano makubwa yaliyoambatana na vurugu na uvunjifu wa amani baada ya wakereketwa wa mrengo wa kulia, kuingia mitaani na kuonyesha chuki dhidi ya wageni na waislamu.
Polisi wamekuwa wakijaribu kutuliza hali kwa kushika doria mitaani huku wakisaidiwa na mbwa.
TRT Afrika