Serikali ilisema itaendelea na juhudi zake za uchunguzi wa mtandao / Picha: Reuters

Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Kenya amethibitisha kufanyika kwa shambulio la mtandao kwenye jukwaa la kidigitali ambalo hutoa huduma za serikali na kushikilia data muhimu ya kibinafsi ya raia.

Jukwaa la eCitizen linahusika na usajili wa data za kibinafsi ikiwa ni pamoja na vitambulisho , pasipoti au hati ya kusafiri, vyeti vya kuzaliwa, leseni za udereva, vibali vya makazi, na usajili wa biashara mpya.

Waharibifu walijaribu kuingilia jukwaa hilo kupitia mzigo mkubwa wa maombi ya data, alisema Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Eliud Owalo, katika kipindi cha redio asubuhi siku ya Alhamisi.

Hakuna data iliyofikiwa au kupotea kwani mfumo haukudukuliwa, na mifumo yote na majukwaa chini ya udhibiti wa serikali ilikuwa salama, alisema katika taarifa ya baadaye.

Hakuna data iliyofikiwa au kupotea kwani mfumo haukudukuliwa, na mifumo yote na majukwaa chini ya udhibiti wa serikali ilikuwa salama, alisema katika taarifa ya baadaye.

Mtandao kuingiliwa

Pia kulikuwa na jaribio lisilofanikiwa la kulenga sekta binafsi, iliongeza.

"Kwangu hilo si jambo geni kwa sababu mashambulizi ya kimtandao yapo duniani kote. Hatuwezi kusitisha kuweka rekodi zetu na huduma zetu kwa mfumo dijitali kwa sababu tunataka kuepuka hatari," Bwana Owalo alisema katika kipindi hicho.

Aliongeza: "Walijaribu kuziba mfumo kwa kufanya maombi zaidi ya kawaida kwenye mfumo. Hivyo mfumo ulianza kupungua kasi, lakini baadaye tulishughulikia hali hiyo."

Waziri alisema hatua za kurekebisha zilichukuliwa kushughulikia hali hiyo na serikali "itaunda hatua za kina za kupunguza hatari kwa ajili ya kudumisha maendelea ya kidijitali."

Watumiaji wa jukwaa la eCitizen wameripoti kusumbuliwa na kushindwa kufanya shughuli kwa muda wote wa wiki.

Pia, siku ya Alhamisi, kumeripotiwa kushindwa kwa shughuli za kutuma pesa za mkononi na huduma za benki za mtandao, ingawa haieleweki ikiwa zilikuwa zimehusiana na shambulio la mtandao kwenye jukwaa la serikali.

Kenya ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zilizo na sheria za usalama wa data na sheria ya ulinza wa taarifa binafsi.

TRT Afrika