Shirika la Viwango la Kenya (KEBS) limewaarifu waagizaji mitumba kwamba magari yaliyosajiliwa mwaka wa 2017 hayataruhusiwa kuingia nchini baada ya Desemba 31, 2024.
Kikomo cha umri kinalenga kuzuia utupaji wa magari machakavu nchini Kenya na baadaye kuimarisha usalama barabarani.
Katika notisi, KEBS iliwashauri waagizaji bidhaa kuwa magari yote yaliyosajiliwa 2017 au mapema lazima yawasili nchini kabla ya muda kwisha ili kuepuka adhabu.
Hatua hiyo, kulingana na KEBS, pia inaathiri wakaazi wanaorejea, wafanyikazi wa kidiplomasia na umma kwa jumla.
"... ni Hifadhi ya upande wa kuendesha ya Kulia tu ( RHD) ya magari ambayo Mwaka wa Usajili wa Kwanza ni kuanzia Januari 1, 2018 na baadaye yataruhusiwa kuingia nchini kuanzia Januari 1, 2025," taarifa ya KEBS ilisoma kwa sehemu.
Zaidi ya hayo, KEBS imesema magari yanayoagizwa kutoka nchi ambako KEBS ina wakala wa ukaguzi yataandamana na cheti cha kuonyesha zinafaa barabarani iliyotolewa na kampuni ya ukaguzi.
Nchi hizo ni pamoja na Japan, Falme za Kiarabu, Uingereza, Thailand, Singapore na Afrika Kusini.
"Gari yoyote ililosajiliwa 2017 au mapema zaidi, itakayowasili baada ya Desemba 31, 2024 itachukuliwa kuwa haiambatani na KS 1515:2000 ( sheria )na itakataliwa kwa gharama ya muagizaji." ripoti ya kEBS imesema.