Maambukizi mengi yameripotiwa katika nchi ya DRC / Picha: AFP

Wizara ya Afya nchini Kenya inaripoti maambukizi ya pili yaliyothibitishwa ya ugonjwa wa Mpox.

Mgonjwa huyo ambaye ni dereva wa lori, alitambuliwa katika Kituo cha Mpakani cha Malaba katika Kaunti ya Busia, akionyesha dalili baada ya kusafiri kutoka kwa kitovu cha mlipuko nchini DRC.

"Mgonjwa ametengwa na yuko chini ya usimamizi madhubuti katika moja wapo ya vituo vyetu vya afya nchini Busia," taarifa ya Wizara ya Afya imesema.

"Ufuatiliaji zaidi wa maambukizi umeimarishwa katika eneo hili na katika kaunti zote unadhibitiwa," imesema ripoti hiyo.

Sampuli kutoka watu 42 zimepelekwa katika maabara kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na 40 hazijapatina na mambukizi.

"Aidha, tumehakiki jumla ya wasafiri 426,438 katika Bandari zetu mbalimbali za kuingia nchini kote," aliongeza.

Haya yanajiri takriban wiki tatu baada ya nchi hiyo kuthibitisha mgonjwa wa kwanza katika mpaka wa Taita Taveta na Tanzania.

Mgonjwa wa kwanza pia alikuwa ni dereva wa gari la mizigo la masafa marefu kutokea Uganda kuelekea Rwanda kupitia Kenya, Wizara ya Afya ilisema wakati huo.

TRT Afrika