Mamlaka ya wanyamapori nchini Kenya, KWS, inasema imeongeza msako wa kumtafuta simba maarufu kama Olobor aliyetoweka tangu Januari mwaka huu. Picha wengine. 

Mamlaka ya Wanyamapori nchini Kenya, KWS, inasema imezidisha msako wa kumtafuta Olobor, simba maarufu wa Hifadhi ya Kitaifa ya Maasai Mara kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Simba huyo maarufu, ni mmoja wa kundi la "Black Rock Lion Pride," ameripotiwa kutoweka tangu katikati mwa mwezi Januari mwaka huu.

Wakati huo huo, KWS imekana madai kuwa huenda simba huyo aliuawa kufuatia ujumbe katika wa mitandao ya kijamii kuwa aliuliwa na wafugaji.

"Vikosi vya kijasusi na uchunguzi vya KWS vimezuru eneo hilo lakini hakuna ushahidi wala taarifa zilizokusanywa kuthibitisha madai hayo," KWS imesema katika taarifa.

"KWS iliwapa jukumu wasimamizi wakuu wa hifadhi hiyo pamoja na kikundi kinachoitwa 'Mara predators' timu ya watafiti ambao kazi yao ya kufuatilia simba ili kumtafuta Olobor.

KWS inasema itatoa maelezo sahihi kwa umma kuhusu Olobor wakati ukweli utathibitishwa.

TRT Afrika