Bodi ya Famasia na Sumu ya Kenya (PPB) imeonya wasafirishaji wa dawa zisizo na leseni, waendesha pikipiki, na watoa huduma za usafiri wa umma dhidi ya kushughulikia dawa bila idhini.
Bodi hiyo inafanya operesheni kwa ushirikiano na Huduma ya Kitaifa ya Polisi.
"Hatua hii iliyoimarishwa inafuatia ukaguzi wa hivi majuzi nchini kote wa vituo vya afya uliolenga kubaini na kushughulikia makosa katika sekta ya dawa,” Julius Kaluai, Mkuu wa Utekelezaji na Ufuatiliaji wa PPB amesema.
Msako huo unafuatia ukaguzi wa hivi majuzi wa nchi nzima wa vituo vya afya uliolenga kubaini na kushughulikia makosa katika sekta ya dawa.
Italenga huduma za wasafirishaji wasio na leseni, waendeshaji pikipiki na watoa huduma za usafiri wa umma.
Kaluai amesema msako huo unalenga kukomesha usambazaji wa dawa zisizofuata kanuni kwa kutekeleza viwango vya udhibiti nchini kote.
Amewaonya wanaokiuka kanuni kuwa ni lazima wafikie viwango vya kitaifa au wachukuliwe hatua.
Bodi hiyo imesema kuwa, taarifa zitakazopatikana katika msako huo zitasaidia kubainisha mwelekeo katika shughuli haramu ya dawa na kuwezesha utekelezaji bora zaidi katika usambazaji wa dawa nchini kwa njia tofauti.