Kenya kwa sasa inanunua mafuta yenye thamani ya takriban dola bilioni moja kila mwaka / Picha: AFP

Kenya inapanga kufanya maongezi na wawekezaji wa serikali na wa kibinafsi kutoka Indonesia kwa ajili ya kupata mbinu za kufanya kilimo kubwa ya mafuta ya alizeti, mafuta ya soya na mafuta ya mawese.

Indonesia ndiyo mzalishaji mkuu duniani wa mafuta ya mawese.

Katika taarifa ambayo imetolewa na wizara hiyo imesema ujumbe kutoka Indonesia unatarajiwa jijini Nairobi wiki ijayo kujadiliana na rais William Ruto na Wizara za Kilimo na Biashara jinsi ya kuisaidi Kenya katika uzalishaji kamilifu, haswa katika kupata mafuta hii nchini.

"Mazungumzo yatahusu kusaidia wakulima katika kaunti teule za Lamu, Kwale Tana River, Homabay, Migori, Kisumu na Busia kupitia mpango wa wakulima na ukulima wa mashamba makubwa," taarifa hiyo imesema.

Kenya kwa sasa inanunua mafuta yenye thamani ya takriban dola bilioni moja kila mwaka kupitia makampuni matano: Bidco, Kapa Oil, Pwani Oil, Menegai na Golden Africa.

"Desemba mwaka jana kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wananachi wakati bei ya mafuta ya kupikia ilipanda hadi takriban dola 3.5 kwa kilo, hii ililazimisha serikali kuagiza mafuta kutoka nje kupitia shirika la biashara la kitaifa la Kenya. Bei ya reja reja ikashuka hadi dola 1.5 kwa kilo," taarifa hiyo imesema.

Kulingana na muungano wa uzalishaji maarufu kama Kenya Manufacturers Association, nchini Kenya sekta ya kuchakata mafuta ya Kula inaundwa na watengenezaji 13 .

Wana uwezo wa pamoja wa uzalishaji na usindikaji wa takriban Tani milioni 2 kwa mwaka.

TRT Afrika