Kenya imehusika katika kulinda amani katika nchi tofauti barani Afrika / Picha:  KDF EACRF 

Kenya inaadhimisha miaka 60 ya kuhusika katika uwanja wa diplomasia.

"Kenya imesalia imara katika kutetea umoja wa kimataifa, mazungumzo na kuheshimiana," seriklai imesema katika taarifa yake. Kama mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Afrika, taifa hilo limekuwa likitetea umoja wa Afrika na ushirikiano wa kiuchumi.

Kenya imekuwa na jukumu muhimu katika juhudi za kimataifa za kulinda amani, ikishiriki katika misheni 43 katika kanda zikiwemo Yugoslavia, Cambodia, Iran, Timor Mashariki na Sahara Magharibi.

Kenya ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Afrika wa mabadiliko ya tabia nchi mwaka 2023/ Picha: Reuters 

Imechangia katika kulinda usalama nchini Sierra Leone, Liberia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Somalia, Sudan Kusini na Haiti, ikichangia katika juhudi za kujitolea kwa utulivu wa kikanda na kimataifa.

Kenya pia imejiimarisha kama kitovu cha diplomasia na maendeleo ya mazingira duniani. Matukio ya kihistoria yamefanyika nchini humo kama vile Mkutano wa Tatu wa Dunia wa Wanawake (1985), Mkutano wa UNEA (2022), Mkutano wa kwanza wa viongozi wa serikali ya Hali ya Hewa Afrika (2023), Mkutano wa Uchumi Endelevu wa Bluu, na Mkutano wa pili wa Umoja wa Mataifa wa Bahari (ulioandaliwa pamoja na Ureno).

Zaidi ya hayo, uchaguzi wa Kenya katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) mwaka 2021 kwa muhula wake wa tatu ulithibitisha jukumu lake muhimu katika kuunda utawala wa kimataifa na kukuza sauti ya Afrika katika diplomasia ya kimataifa.

Serikali hiyo imesema uchaguzi wa Kenya katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) mwaka wa 2021 kwa muhula wake wa tatu ulithibitisha jukumu lake muhimu katika kuunda utawala wa kimataifa na kukuza sauti ya Afrika katika diplomasia ya kimataifa.

Katika Umoja wa Afrika, Kenya imekuwa mwanachama wa Tume ya Amani na Usalama.

Mwaka 2024 Rais William Ruto ameidhinishwa kuongoza juhudi za Umoja wa Afrika wa Mageuzi ya Kitaasisi ya AU.

Pia inagombea uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika katika uchaguzi unaofaa kufanywa na marais Februari 2025.

TRT Afrika