Kenya protests

Serikali imetoa onyo kwa wanaopanga kushiriki maandamano kufuata utaratibu wa kisheria ikiwemo kuheshimu mali na biashara za raia.

Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amewataka vijana hao kuimarisha amani na wasibebe silaha zozote, nalazima wawe wameondoka kufikia saa kumi nambili jioni.

''Vyovyote vile, malalamiko yoyote, jambo lolote, utawala wa sheria na utulivu wa umma lazima udumishwe na wote,'' alisema Waziri Kindiki katika taarifa yake.

Kufikia saa mbili asubuhi polisi walikuwa tayamri wameshika doria katika barabara kadaa za kati kati ya jiji la Nairobi ambako kunatazamiwa kuwa kitovu cha maandamano hayo, huku sehemu ya mji ukifungwa hasa kuelekea maeneo ya bunge.

Wasafiri pia walitatizika alfajiri kwani baadhi ya barabara zilionekana wazi kabisa kwa upungufu wa magari na mabasi ya umma kwa hofu ya maandamano hayo.

Azma kali ya mabadiliko

Vijana waliotambulika kama Gen Z wamekuwa wakifanya maandamano kwa siku kadhaa nchini Kenya kupinga mswada wa fedha 2024 unaodaiwa kulimbikiza ushuru zaidi kwa raia.

Tangu mwanzo wa maandamano, viongozi wengi waliwashutumu vijana hao kwa kuchochewa kuitisha mabadiliko kwa mambo wasio elewa, wakiashiria kuwa wengi wao hawakuwana ufahamu wowote juu ya sheria hiyo.

Hata hivyo wengi wa viongozi hao wamelazimika kuomba msamaha hadharani kwa matamshi yao na kuahidi kushirikiana na vijana katika majadiliano ya kutafutia suluhu mswada huo.

Rais Ruto ni miongoni mwa viongozi waliolainisha msimamo wao juu ya tetesi hizo na kuahidi kuitisha vikao na vijana.

Hata hivyo baadhi waliojibu katik amitandao ya kijamii wamesema kuwa hayo yamepitwa na wakati huku wakidai kutupwa kabisa kwa mswada huo badala ya kubadilishwa vipengee kadhaa kama inavyopendekezwa na wabunge.

Kulinda haki za waandamanaji.

Huku taifa nzima la kenya likijiandaa kwa maandamano hayo, wanaharakati wa haki zabinadamu wamelalamikia hatua ya kukamatwa kiholela kwa baadhi ya vijana waliotambuliwa kushiriki maandamano hayo.

Malalmiko hayo yanaungwa mkono na maelfu ya vijana mtandaoni walioelezea hofu ya kulengwa na kukamtwa na polisi kuhujumju maandamano yao.

Chama cha wanasheria nchini Kenya LSK kimesema katika kuwa hatua ya kuwakamata waandamanaji inairudisha Kenya katika enzi za utawala wa kidikteta.

''Katika saa 72 zilizopita, Kenya imerudishwa nyuma kwenye enzi ya giza ya uongozi wa kitapeli na uzembe,'' aliandika fait Odhiambo, Rais wa Chama hicho. ''Jeshi la polisi linalofanya kazi kwa njia ya ukandamizaji, kisiri, kinyume cha sheria, nje ya mahakama, ni mbinu za kuzima kwa nguvu upinzani wa umma dhidi ya mashaka ya serikali,'' aliongeza kusema.

Wasiwasi ulizidi baada ya video kadhaa za CCTV kutolewa zikionyesa baadhi ya wanaharakati waliovuma zaidi katika maandamano hayo wakivamiwa na kutekwa na watu waliovalia nguo za raia.

Baadhi waliotekwa wameachiliwa bila mashtaka yyoyote baada ya kuzuiliwa kwa muda katika wanachosema ni ofisi za idara ya upelelezi.

Maandamano yanayoongozwa na Gen Z, yamezua wasiwasi miongoni mwa wanasiasa wakongwe huku wengine wakishutumu kama uchpchezi .

Lakini pia yamevutia pongezi mtandaoni kutoka ndani na nje ya nchi kuwa ishara ya uamsho wa vijana kwa maslahi ya maisha yao na uongozi.

TRT Afrika