Kenya ina changamoto ya chanjo kwa watoto baada ya serikali kukosa kununua chanjo za kutosha kwa muda uliofaa. Nchi ilikosa kusambaza chanjo kwa mwaka mzima baada ya kushindwa kulipa deni la zaidi ya dola za Marekani milioni 15, ambazo ni sawa na shilingi bilioni mbili kwa muuzaji wa kimataifa.
Hatua hii inasemekana itaathiri takriban watoto wachanga milioni 1.6, idadi hii ya kina mama waja wazito na zaidi ya wasichana 750,000 chini ya umri wa miaka 10.
"Wizara ya afya imetenga dola za Marekani zaidi ya milioni 1.9 ( shilingi milioni 250 ) kununua dawa za kawaida za antijeni na kujaza chanjo ya kuokoa maisha katika vituo vyetu vya afya," Wizara ya Afya imesema katika taarifa kwa waandishi wa habari.
Chanjo ya BCG, ambayo hupewa mtoto akizaliwa kwa ajili ya kuzuia kifua kikuu, haijanunuliwa kwa miezi minane.
"Licha ya changamoto kutoka msimu wa mvua sasa wizara na washirika wake wanaharakisha usafirishaji wa chanjo inayotarajiwa kuingia nchini mwanzo wa Juni 2024," Wizara hiyo imeongezea.
Kenya pia haijanunua chanjo ya DTP (Diphtheria, Tetanus, na Pertussis) kwa muda wa miezi 10, huku kukiwa na ripoti kuwa hospitali za umma zina uhaba.
Tayari, TB, polio, surua, rubela, pneumococcal conjugate chanjo (PCV), rotavirus, chanjo ya polio ambayo haijawashwa (IPV), surua-rubela (MR), human papillomavirus (HPV), chanjo ya homa ya manjano na chanjo ya malaria hazipo.
Chanjo ya HPV hutolewa kwa wasichana chini ya miaka 10 na ambao wanafikia takriban 750,000 kila mwaka.
Nchi inatarajiwa kuwa na akiba angalau miezi nane ya kila chanjo kwa kila wakati.