Kenya kusitisha makubaliano na madaktari wa Cuba: Waziri wa Afya Susan Nakumicha. Picha: Wizara ya Afya

Waziri wa Afya nchini Kenya, Nakumicha S. Wafula, ametangaza kuwa serikali ya nchi hiyo imesitisha mkataba wake na madaktari wa Cuba.

Serikali hiyo imeongeza kuwa haitarefusha makubaliano yake na madaktari wa Cuba ambao wamekuwa nchini Kenya tangu mwaka 2017 pindi serikali za za mataifa hayo mawili zilipoafikiana kuruhusu madaktari 100 wa Cuba kutoa huduma katika hospitali za Kenya.

Nakumicha ameyasema hayo wakati akiwahutubia wataalamu wa afya katika ufunguzi rasmi wa kongamano la mazungumzo ya rasilimali watu ya kitaifa yenye lengo la kuboresha huduma za afya nchini humo.

"Kama wizara, nina hakika kwamba tutakuwa na nguvu kazi yenye motisha," Waziri alisema na kuongeza, "Wataalamu wetu wa afya wamejitolea kufanikisha hilo.”

Kongamano hilo linajumuisha majadilanio ya kutathmini mazingira ya sasa ya wafanyakazi wa sekta ya afya na changamoto zinazoathiri utoaji wa huduma kwa jumla.

TRT Afrika