Kenya inafanya kampeni dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa kugawa vyandarua za kukinga malaria.
Malaria ni ugonjwa hatari unaoenezwa kwa binadamu na baadhi ya aina za mbu.
Malaria ina tiba na inaweza kukingika kwa kutimia mbinu kama vyandarua.
Wizara ya Afya ya Kenya inasema inagawa vyandarua ambavyo zinaweza kukaa na dawa kwa muda mrefu.
"Kampeni inawakilisha hatua madhubuti kuelekea lengo la upatikanaji wa neti kwa wote kwani serikali inalenga kusambaza neti milioni 15.3 katika kaunti 22 zenye hatari kubwa ya malaria," anasema Mary Muthoni, katibu mkuu wa Idara ya Afya.
Vyandarua hutengeza kizuizi cha kinga karibu na watu wanaolala chini yake.
Wizara ya Afya inasema kiwango cha malaria nchini kimepungua lakini bado kuna changamoto hasa katika maeneo kando ya Ziwa Victoria na Bonde la Ufa.
"Kupungua kwa maambukizi ya malaria kutoka 11% mwaka 2015 hadi 6% ya sasa kunaashiria maendeleo lakini changamoto zinaendelea kwani malaria bado inachangia kati ya 13 % na18% ya wagonjwa wanaofika katika vituo vya afya nchini," Muthoni ameongezea.
Hata hivyo, vyandarua vilivyotiwa dawa ni kinga zaidi kuliko vyandarua visivyotibiwa.
Umuhimu wa neti
Kuna vyandarua aina tofauti.
Kwa sasa Shirika la Afya Duniani, linasema ni bora kwa wananchi kutumia neti zinazoweka dawa kwa muda mrefu yaani.
WHO inasema vyandarua hivyo ni bora zaidi kuliko neti ambazo hazijatibiwa kwa sababu zinatengenezwa kwa vyandarua ambavyo vina dawa ya kuua wadudu inayopendekezwa na WHO.
Wataalamu wa afya wanasema athari ya mbu hudumu kwa muda mrefu na neti zinaweza kutumika hadi miaka mitatu au baada ya kusafishwa mara 20.
Hapo awali, vyandarua vililazimika kurudishwa kila baada ya miezi 6 hadi 12, au hata mara nyingi zaidi ikiwa vyandarua vilioshwa.
Mtu alikuwa akilazimika kuvitumbukiza kwenye mchanganyiko wa maji na dawa ya kuua wadudu na kuziruhusu kukauka mahali penye kivuli.
Haja ya kurudishwa mara kwa mara ilikuwa kikwazo kikubwa kwa matumizi makubwa ya vyandarua katika nchi zenye changamoto ya malaria.
Makampuni kadhaa yametengeneza vyandarua vyenye dawa ya kudumu kwa angalau miaka mitatu hata baada ya kuosha mara kwa mara.
WHO inapendekeza kuwa vyandarua hivi vitolewe bure.