Jaji Mkuu wa Kenya Martha Koome amesema kuwa ni wakati muafaka kuhakikisha kuna ufahamu wa kutosha kabla ya kukamatwa kwa unaofaa kabla ya watu kukamatwa na polisi.
" Labda ni wakati wa Jeshi la Polisi la Taifa kuweka kanuni za kuamua nani anaamua kushtakiwa na kukamtwa. Tunapokamata, ni lazima kulinda uhai kwani uhai muhimu," amesema Koome.
Ripoti ya Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya, inaonesha kuwa watu 50 waliuwawa katika maandamano yalioanza nchini Kenya, Juni 18, 2024.
" Licha ya polisi kutumia nguvu za kinyama, tutaendelea kudai kuwajibishwa kwa vifo, majeraha na utekaji nyara waliosababisha wakati wa maandamano ya hivi majuzi nchini Kenya. Waliokamatwa leo (25 Julai 2024) na waliotekwa nyara hapo awali lazima waachiliwe bila masharti," Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya imesema.
Polisi wamelaumiwa kwa kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.
Jaji Mkuu amesema kuwa ni muhimu vitengo vya sheria na usalama vifanye kazi inavyofaa kwani wananchi wa sasa wanadai maafisa husika wawajibike ipasavyo.
Waandamanaji waliwatambua baadhi ya Polisi ambao wanadaiwa kutumia nguvu kuwanyanyasa waandamanaji. Hata hivyo, hakuna aliyekamatwa wala kufikishwa mahakamani mpaka sasa.
IPOA yalaumiwa kushindwa kuwawajibisha waliofanya makosa
" Tunataka umma ujue tunafanya kazi katika mazingira magumu sana. Katika historia ya IPOA , hatujawi kushuhudia kiwango cha chini cha ushirikiano kutoka maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi,” John Waiganjo, Kamishna wa IPOA amesema katika mahojiano na vyombo vya habari.