Mdhibiti wa dawa Kenya anarudisha mzigo wa dawa ya kikohozi la sirapu ya watoto ya Johnson & Johnson, ilisema Alhamisi, siku moja baada ya Nigeria kuondoa aina hiyo ya dawa sokoni ambayo iko chini ya kampuni ya Benylin Paediatric.
Mdhibiti wa afya wa Nigeria alisema kuwa vipimo vya maabara vilivyo fanyika kwenye sirapu hiyo vilionyesha kiwango cha juu cha diethylene glycol, ambacho kimehusishwa na vifo vya makumi ya watoto nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu 2022 katika moja ya milipuko mibaya zaidi ya sumu kusababishwa na dawa za kumeza duniani.
"Uchambuzi wa maabara uliofanywa kwenye bidhaa hiyo ulionyesha kuwa ina kiwango kisichokubalika cha juu cha Diethylene glycol na iligundulika kusababisha sumu kali ya mdomo kwa wanyama wa maabara," alisema Afisa wa Kitaifa wa Udhibiti wa Chakula na Dawa wa Nigeria (NAFDAC).
Bodi ya Dawa na Sumu ya Kenya (PPB) ilisema katika taarifa kuwa imeanza uchunguzi na imeshauri kwamba mauzo ya mizigo za bidhaa hiyo zisitishwe na zirudishwe kwa wauzaji.
Kenvue, ambayo sasa inamiliki chapa ya Benylin baada ya kutengana na J&J mwaka jana, haikujibu mara moja ombi la kutoa maoni.
Mzigo unaorudishwa ulitengenezwa na J&J nchini Afrika Kusini mnamo Mei 2021 ikiwa na tarehe ya mwisho wa matumizi ya Aprili 2024, PPB ilisema.