Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemsifu mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan kwa jitihada zake za utunzaji wa mazingira, na kumshukuru kwa "uongozi wake katika maeneo muhimu kama utunzaji wa mazingira."
Katika ujumbe wake, Guterres ameishukuru Uturuki kwa kuwa mwenyeji wa mkutano kwa kushirikiana na mpango wa Umoja wa Mataifa wa mazingira na Umoja wa Mataifa unaoshughulikia Makazi, na kusema, "Namshukuru Emine Erdogan, Mke wa Rais wa Uturuki, kwa uongozi wake wenye maono kwenye maeneo ya utunzaji wa mazingira," katika ujumbe wa video uliotumwa Machi 30, Siku ya Utunzaji wa Mazingira iliyofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Jumamosi.
Guterres pia amesema kwamba bodi ya ushauri ya mazingira imekuwa ikileta washirika pamoja tangu mwaka jana kuzungumzia changamoto hiyo.
"Katika viwango vyote, serikali zinatakiwa kuwekeza katika mipango ya menejimenti ya uchavu kwa kujikita katika kutumia upya, na kuepusha uchafu, na kujenga uchumi unaozingatia uzungushaji wa taka na matumizi ya rasilimali," amesema.
"Jamii ya kimataifa inaungana kama chombo kimoja na kufanya kazi kuelekea kuweka saini makubaliano ya kisheria yatakayotokomeza uharibifu wa mazingira kupitia plastiki."
Mke wa Rais wa Uturuki ameongoza vuguvuru ya kupambana na uharibifu ya mazingira nchini Uturuki na kusaidia kuukuza katika kiwango cha kimataifa, na kuchochea Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Disemba 2022 kupitisha azimio la kuunga mkono misingi ya jitihada hizo.
Kwa mujibu wa UN, siku ya kimataifa ya kutokomeza uchafu inakuza uwajibikaji katika uzalishaji kwa kuzingatia mabadiliko kuelekea mtizamo tofauti.