Mwendesha Mashtaka huyo amewasili nchini DRC huku taifa hilo likiwa limeghubikwa na machafuko katika eneo la Mashariki./Picha: Reuters      

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Karim Khan yupo nchini DRC, ofisi yake imesema.

Mwendesha Mashtaka huyo amewasili nchini DRC huku taifa hilo likiwa limeghubikwa na machafuko katika eneo la Mashariki.

Hivi karibuni, kikundi cha waasi cha M23 kinachoungwa mkono na Rwanda, kilidhibiti maeneo muhimu ya nchi hiyo.

"Tuna wasiwasi mkubwa na hali ya usalama inavyoendelea nchini DRC," alisema Khan, mara tu baada ya kuwasili jijini Kinshasa.

"Ujumbe uko wazi kabisa, kikundi chochote kile hakina haki kutekeleza kile kinachoendelea," alieleza.

Janga la kibinadamu

"Ni lazima sheria za kimataifa za haki za kibanadamu zizingatiwe," Khan aliongeza.

Kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa, kundi la M23 linaungwa mkono na wanajeshi wapatao 4,000 kutoka Rwanda.

TRT Afrika