Vita kati ya jeshi la Sudan linaloongozwa na jenerali  Mohamed Hamdan Dagalo na jenerali Abdel Fattah al-Burhan vilianza Aprili 15.   

Mawaziri wa kutoka Kenya, Djibouti, Ethiopia na Sudan Kusini walifanya mkutano wa mtandawo Jumatatu, kwa ajili ya kuanza kufanya mipango ya kurejesha amani katika Jamhuri ya Sudan.

Vita kati ya jeshi la Sudan linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na mpinzani wake wa kikundi cha Rapid Support Forces, RSF, kinachoongozwa na jenerali Mohamed Hamdan Dagalo vilianza Aprili 15.

Mawaziri wa IGAD wameamua kuteua mjumbe maalum kwa ajili ya kuongoza mchakato wa kikanda wa amani nchini humo.

Waliamua kuhakikisha kuwa Sudan inapewa heshima ya umiliki na uongozi wa mchakato wa amani utakaoamuliwa.

Umoja wa Afrika pia itahusishwa kwa karibu katika mipango yote ya IGAD ya kujaribu kuleta amani Sudan.

Marais wa IGAD waliteua rais wa Kenya William Ruto kama kiongozi wa kamati hii ya amani lakini Sudan imemkataa na kudai kuwa Kenya inaunga mkono kikundi cha Rapid Support Forces ambacho kinapigana na jeshi la Sudan tangu 15 Aprili.

TRT Afrika