Wananchi wa Sudan na jamii ya kimataifa waaangalia kwa matumaini makubwa utimizaji wa mkataba mpya wa kusitisha vita kuanzia Jumatatu saa nne kasorobo usiku nchini Sudan.
Wanajeshi wa Sudan na vikosi vya Rapid Support Forces ambavyo vimepigana tangu tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu, vilikubaliana kuhakikisha usafirishaji wa huduma ya kibinadamu nchini sudan kwa siku saba.
"Ni wakati wa pande zinazopigana kunyamazisha bunduki, kuruhusu utoaji salama wa misaada ya kibinadamu, na kurejesha huduma muhimu. Sisi na washirika wetu tutaendelea kufanya kila tuwezalo ,” Martin Griffiths, mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu na mratibu wa misaada ya dharura.
Tofauti na majaribio ya awali ya kusitisha mapigano hii ina utaratibu wa kimataifa wa ufuatiliaji.
"Heshima ya usitishaji vita ni muhimu kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa misaada kwa zaidi ya watu milioni 25 wa Sudan ambao wana mahitaji makubwa, ambayo ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu wa nchi," Utaratibu wa pande tatu ambao unajumuisha Umoja wa Mataifa, umoja wa Afrika na IGAD na Umoja wa Mataifa unasema katika taarifa yake.
Lakini ni majaribio gani yamefanywa ya kusitisha mapigano nchini Sudan tangu tarehe 15 mwezi mei mwaka huu?
Tarehe 16 mwezi Aprili mwaka huu Mwakilishi Maalum wa Umoja wa mataifa nchini Sudan alipendekeza pande zinazopigana kukubaliana na kusitisha vita kwa muda tarehe 16 Aprili kati ya saa kumi jioni na saa na moja usiku .
Lakini hii haikuheshimiwa kikamilifu na pande zote mbili.
Uratibu wa pande tatu ambao unajumuisha Umoja wa Mataifa, IGAD na Umoja wa Afrika uliomba pande mbili kusitisha vita tarehe 17 Aprili , bila kufaulu.
Mashirika haya yalifanya juhudu tena kushawishi pande zinazopigana kusitisha vita tarehe 19 Mei, kuanzia saa kumi na mbili jioni - kwa masaa ishirini na manne , lakini hii haikufaulu.
Mashirika haya yalifanya juhudu tena kushawishi pande zinazopigana kusitisha vita tarehe 19 kuanzia saa kumi na mbili jioni - kwa masaa ishirini na manne , lakini hii haikufaulu.
Tarehe 20 Aprili , katibu mkuu wa Umoja wa mataifa na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika waliomba vita visitishwe kutoka usiku wa manane wa tarehe 20 had tarehe 23 mwezi Aprili kwa heshima ya Eid al- Fitr ,
Tarehe 24 chini ya upatanishi wa Marekani , pande zinazozozana zilikubali kusitisha vita kwa masaa 72 . Lakini vita vikaendelea kuripotiwa.
Tarehe 27 mwezi Aprili Marekani na Saudi Arabia ziliongoza mapatanisho kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya Rapid Support Forces kwa masaa mengine 72.
Tarehe 2 mwezi Mei, rais wa Sudan kusini Salva Kiir alitangaza kuwa pande zote mbili zilikuwa zimemekubaliana kusitisha vita kati ya tarehe 4 na tahere 11 mwezi Mei. Lakini haikutimizwa.
Tarehe 6 mwezi Mei wawakilishi wa vikundi zinavyopigana vilikutana kwa ajili ya kupanga mapatanisho.
Tarehe 11 Mei pande hizi mbili zilitia saini makubaliano ya usitishaji vita kwa ajili ya kusafirisha mahitaji na huduma za kibinadamu kwa waliathiriwa na vita .
Na sasa kuna makubaliano mapya ambayo yanaanza tarehe 22 Mei kwa ajili ya usafirishaji wa huduma za kibinadamu .