Jamhuri ya Congo yathibitisha maambukizi mapya 21 ya 'homa ya nyani'

Jamhuri ya Congo yathibitisha maambukizi mapya 21 ya 'homa ya nyani'

Taarifa hizo zimetolewa na Waziri wa Afya wa nchi hiyo siku ya Jumapili.
Maambukizi mapya 21 yamethibitishwa katika jamhuri ya Congo./Picha:  AFP

Waziri wa Afya wa nchi hiyo ameuthibitishia umma juu ya uwepo wa maambukizi mapya 21 ya ugonjwa wa Mpox.

Gilbert Mokoki alisema kuwa nchi hiyo inayopatikana Afrika ya kati "imeripoti maambukizi 158, tangu mwanzoni mwa mwaka 2024.

Ripoti za maambukizi ya ugonjwa huo zimekuwa zikiongezeka mashariki na kati mwa Afrika, vikigundulika pia Asia na Ulaya, huku Shirika la Afya Ulimwenguni likitangaza hali ya dharura.

Kirusi kipya cha mpox

Virusi hivyo vimeripotiwa katika mikoa mitano kati ya 15 ya Congo-Brazzaville, huku maeneo ya misitu ya Sangha na Likouala kaskazini yakiathirika zaidi.

Kirusi hicho kimeenea pia katika nchi ya jirani ya DRC, ikiua zaidi ya watu 570, mwaka huu.

Japo si hali ya kutisha nchini Congo-Brazzaville, Mokoki alitoa wito kwa watu kuchukua hatua za kujikinga kama vile kunawa mikono mara kwa mara.

TRT Afrika