Senegal inasema homa ya mafua ya ndege ya H5N1 huenda ikaenea kutoka kwa ndege wa porini hadi kwa mifugo Picha: Anadolu Agency / Poto: AA

Wizara ya mifugo ya Senegal imeripoti kuzuka kwa homa ya ndege ya H5N1 yenye kusababisha magonjwa mengi.

Shamba la kuku katika kijiji cha Potou karibu na mji wa Kaskazini-Magharibi wa Louga ndio hivi karibuni limekumbwa na mlipuko huo ambapo ndege 500 walioripotiwa kubeba homa ya H5N1, wizara ilisema Ijumaa.

Mamlaka ilisema pia imeua takriban ndege 1,229 kufikia sasa katika Hifadhi ya Langue de Barbarie na maeneo jirani.

Homa ya mafua ya ndege aina ya A H5N1 "iligunduliwa kwa mara ya kwanza Machi 8 kutokana na sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa ndege wa kifalme wanaozunguka Ziwa Pinki, na Kisiwa cha Yoff karibu na mji mkuu wa Dakar," iliongeza.

Katika Ziwa Pinki, vifo vya ndege 323 vimerekodiwa, wakati katika Kisiwa cha Yoff, ndege 213 walikufa.

Wizara ya mifugo nchini Senegal ilisema "kuna uwezekano mkubwa kwamba virusi vilienezwa na ndege wanaohama," iliongeza.

Hatari kwa wanadamu

Homa ya mafua ya ndege au homa ya ndege imekuwa ikienea duniani kote katika mwaka uliopita, na kuua zaidi ya ndege milioni 200, kulingana na ripoti ya Shirika la Dunia la Afya ya Wanyama.

Watu wanaweza kupata virusi kwa kuwasiliana na ndege walioambukizwa lakini maambukizi ya binadamu hadi kwa binadamu si ya kawaida. Picha/Reuters

Shirika la Afya Duniani, WHO, inasema maambukizi ya H5N1 kwa binadamu yanaweza kuwa makali na kuwa na kiwango cha juu cha vifo.

Lakini inasema virusi hivyo haviambukizi binadamu kwa urahisi, na husambaa kutoka kwa mtu hadi mtu ''inaonekana kuwa isiyo ya kawaida.''

Iliongeza kuwa takriban visa vyote vya maambukizi ya H5N1 kwa watu ''vimehusishwa na kugusana kwa karibu na ndege walioambukizwa au waliokufa, au mazingira yenye virusi vya H5N1.''

Lakini kumekuwa hakuna ushahidi kwamba watu wanaweza kuambukizwa kupitia ''chakula kiliyoandaliwa vyema na kupikwa vizuri,'' Shirika la Afya duniani lilisema.

Lakini ilionya kwamba ikiwa virusi vya H5N1 vingebadili tabia yake na kuambukizwa kwa urahisi miongoni mwa watu huku vikibaki na uwezo wake wa kusababisha ugonjwa mbaya, ''matokeo kwa afya ya umma yanaweza kuwa makubwa sana.''

TRT Afrika na mashirika ya habari