Kati ya watu biliioni 8, watu bilioni moja ni wanene, kulingana na utafiti uliofanywa na Lancert. / Picha: AFP

Na Sylvia Chebet

TRT Afrika, Istanbul, Uturuki

Kunenepa sana sio tu kushindwa kuficha manyama uzembe au kutotoshea kwenye nguo. Sasa ni janga la afya duniani ambalo linaonekana wazi lakini mara nyingi hupuuzwa.

Utafiti mpya uliofanywa na The Lancet unaonyesha kuwa kufikia mwaka 2022, zaidi ya watu bilioni moja duniani kote watakuwa na unene uliopita kiasi.

Data iliyokusanywa kutoka nchi 200 au baadhi ya maeneo katika miongo mitatu iliyopita pia inaonyesha kuwa asilimia 43 ya watu wazima duniani wana uzito kupita kiasi.

Kwa hivyo, kwa nini ulimwengu unazidi kuwa na watu wanene uliopita kiasi?

Kulingana na Dk Francesco Branca, mwandishi mwenza wa utafiti huo na mkurugenzi wa idara ya lishe na usalama wa chakula ya Shirika la Afya Duniani, ni siri iliyo wazi.

"Mifumo ya chakula imepitia mabadiliko makubwa duniani. Vyakula ambavyo vina mafuta mengi na sukari au vyakula vilivyowekwa kwenye makopo sasa vinatumiwa kila mahali," Dk Branca anaiambia TRT Afrika. "Zina bei nafuu, zinapatikana masaa 24 na zimekuzwa sana, hasa miongoni mwa watoto."

Vyakula vya kupikwa kwa haraka, kulala bila mpangilio, viwango vya juu vya msongo wa mawazo na kukaa bila kufanya mazoezi ya mwili, vimesababisha unene uliopita kiasi.

Vyakula vya kupikwa kwa haraka vinasababisha unene uliopita kiasi. / Picha: Reuters

Inaanzia kwenye umri mdogo

Wataalamu wanabainisha kwa wasiwasi kwamba tatizo la unene wa kupita kiasi linazidi kuanza mapema katika maisha ya watu.

Ripoti ya Lancet inasema kwamba tangu 1990, viwango vya unene wa kupita kiasi vimeongezeka mara nne miongoni mwa watoto na vijana.

"Kusambzwa na kukuzwa kwa maziwa ya watoto wachanga kunachangia janga la unene wa kupita kiasi. Tumegundua kuwa watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee wana hatari ndogo ya kupata unene," anasema Dk Branca.

Ushahidi wa kisayansi unaunga mkono uhusiano kati ya maziwa ya mama na uwezo wa kudumisha uzito wa mwili wenye afya.

"Hao (watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama) pengine wanaweza kukabiliana na mahitaji ya miili yao na kudhibiti vyema ulaji wao wa nishati. Kwa bahati mbaya, matumizi ya vinywaji vyenye sukari, katika umri mdogo ni mojawapo ya vichochezi vya unene wa kupita kiasi," anasema afisa huyo wa WHO.

Tatizo la unene wa kupita kiasi Afrika

Utafiti wa Lancet unaonyesha mabadiliko ya mwili kutoka kwa uwembamba hadi unene yamekithiri katika nchi nyingi, haswa katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Nchi hizi sasa zinarekodi kiwango cha juu cha unene wa kupita kiasi kuliko hata zile nchi zilizoendelea kiuchumi.

"Unene ni tatizo kwa nchi za kipato cha chini na cha kati ambazo zinakabiliwa na mabadiliko ya mtindo wa maisha. Kuwa na watu wengi zaidi ni changamoto kubwa kwa mifumo ya afya ya Afrika, ambayo tayari inakumbwa na matatizo ya kiafya unaosababishwa na upungufu wa lishe," Dk Branca anabainisha.

"Watu wanaoishi na unene wanaweza hata kukabiliwa na matatizo katika kutafuta ajira. Tunakadiria kuwa kutakuwa na hasara ya asilimia 3 ya Pato la Taifa kutokana na janga la unene."

Katika bara la Afrika, Misri ina viwango vya juu vya unene wa kupita kiasi kupita nchi zote. Utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 59 ya wanawake wa Misri wana unene wa kupita kiasi, ikishikilia nafasi ya tisa duniani kote. Huku asilimia 32 ya idadi ya wanaume iko katika jamii ya watu wanene, ikishika nafasi ya 33 ulimwenguni.

"Tumeona ongezeko la kasi la unene wa kupita kiasi Kaskazini na Afrika Kusini. Pia linatambuliwa kama tatizo kubwa katika Afrika Magharibi, hasa nchi kama Nigeria," anasema Dk Branca.

Kwa bahati nzuri eneo la Pembe ya Afrika, hadi sasa imeepushwa na janga la unene uliopita kiasi.

Magonjwa yanayohusishwa na unene uliopita kiasi

Kuongezeka kwa unene na kusababisha unene wa kupita kiasi husababisha vifo milioni tano duniani kote kila mwaka. Magonjwa mengi ya muda mrefu kama vile kisukari na ugonjwa wa moyo na mishipa, pamoja na aina fulani za saratani, yanahusishwa na unene uliopita kiasi.

Utafiti wa Lancet unaangazia umuhimu wa kuzuia na kudhibiti unene kuanzia maisha ya utotoni hadi utu uzima.

Madaktari wanaona kuwa sababu za ugonjwa wa kisukari na hatua za kuidhibiti zinaeleweka vyema, lakini utekelezaji unasalia kuwa changamoto kubwa zaidi.

"Ni jambo ambalo tunaweza kuanza leo, kuhakikisha mlo wetu ni bora zaidi. Tumia nafaka nyingi zaidi, matunda na mboga mboga. Punguza sukari na vinywaji vyenye sukari. Hebu tunywe maji. Hicho ndicho tunachohitaji," Dk Branca anaiambia TRT Afrika.

"Kuwa mkakmavu, tembea badala ya kutumia gari, hata kwa umbali mfupi. Sio lazima kushiriki kwenye mchezo, lakini unaweza kutembea tembea, kwenda kazini kwa miguu, na kucheza na watoto wako."

Katika Mkutano wa Afya Ulimwenguni mnamo 2022, nchi wanachama zilipitisha Mpango wa shirika la afya duniani WHO wa kukomesha unene, ambao unaunga mkono mipango ya nchi 2030.

"Kufikia malengo ya kimataifa ya kupunguza unene kunahitaji ushirikiano wa serikali na jamii...Muhimu zaidi, kunahitaji ushirikiano wa sekta binafsi, ambayo lazima iwajibike kwa madhara ya kiafya yanayosababishwa na bidhaa zao," mkurugenzi mkuu, Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema.

Katika mpangilio, nchi zinapaswa kuhakikisha kuwa mifumo ya afya inaunganisha uzuiaji na udhibiti wa unene kuwa msingi wa huduma.

Kugundua alama za unene

Mzunguko bora wa kiuno kwa wanawake wazima ni 80cm na 90cm kwa wanaume wazima. Picha: Picha za Getty

Kufuatilia molekuli ya mwili (BMI), kupima uzito na urefu wa mtu binafsi, kisayansi ni njia bora ya kudhibiti uzito.

Wakati molekuli mwili wa mtu inazidi 25, ni ishara ya unene wa kupita kiasi. Inapokaribia 30, hiyo ndiyo kengele ya kunenepa kupita kiasi na hatari kubwa ya ugonjwa na kifo cha mapema.

Njia nyingine nzuri ya kufuatilia uzito ni kuangalia mduara wa kiuno. Mzunguko wa kiuno, unaopendekezwa ni sentimita 80 kwa wanawake, na sentimita 90 kwa wanaume. Chochote kilicho juu ya vipimo hivi ni mojawapo ya ishara za uhakika za kupata unene wa kupita kiasi.

"Hiyo pia inamaanisha mafuta ya uzembe itakuwa kubwa na kuwa karibu na tumbo lako. Hatimaye yanaleta hatari kubwa ya kupata kisukari cha aina ya 2, kwa mfano," anaelezea Dk Branca.

Anashauri kutafuta usaidizi wa kimatibabu kwa wale ambao tayari wanakabiliwa na unene uliopita kiasi.

"Hawapaswi kuona aibu," mtaalam wa WHO anaiambia TRT Afrika. "Wala watu wengine hawapaswi kuwalaumu. Mtaalamu wa matibabu anaweza kutoa ushauri unaofaa na kupendekeza aina za lishe na mazoezi ambayo husaidia kupunguza unene."

UNENE WA KUPITA KIASI AFRIKA

Wanawake

Misri 59%

Libya 48%

Afrika Kusini 48%

Eswatini 45%

Ushelisheli 41%

Wanaume

Misri 32%

Libya 28%

Ushelisheli 21%

Eswatini 16%

Afrika Kusini 15%

TRT Afrika