Idara ya Huduma za Ulinzi ya Palestina imesema kuwa majeshi ya Israeli yameharibu zaidi ya makazi 300 huko Jabalia kaskazini mwa Gaza, huku mapigano makubwa yakiendelea kughubika jiji la Rafah.
Msemaji wa idara hiyo Mahmoud Basal ameliambia shirika la Habari la Anadolu kuwa "majeshi ya Israeli yameharibu kabisa zaidi ya makazi 300 huko Jabalia toka kuanza kwa uvamizi wake.”
"Tunapokea taarifa nyingi za uwepo wa miili mingi barabarani na mingine ikiwa kwenye vifusi vya nyumba hizo," alisema huku akiongeza kuwa “vikosi vya uokoaji vinashindwa kufika eneo hilo kutokana na uzito wa mashambulizi ya majeshi ya Israeli."
Basal alieleza kuwa mashambulizi ya Israeli yamesababisha uharibifu mkubwa kwenye maeneo ya makazi katika mji wa Jabalia.
TRT Afrika