Hamas imetoa maelezo kuhusu makubaliano yaliyofikiwa kati yake na Israeli ya kusitisha mapigano baada ya mazungumzo ya muda mrefu.
"Kwa ajili ya wagonjwa wetu na Wapalestina wenye ujasiri, tunaunga mkono Gaza bila kuyumba, kutoa msaada, kuwezesha uponyaji, na kuimarisha upinzani dhidi ya Israeli," Hamas ilisema katika taarifa yake Jumatano.
"Baada ya mazungumzo magumu yaliyofanyika kwa siku kadhaa, tunatangaza, kwa msaada na mafanikio ya Mwenyezi Mungu, kwamba tumefikia makubaliano ya amani ya kibinadamu (kusitisha mapigano kwa muda) kwa kipindi cha siku nne, shukrani kwa juhudi zinazoendelea na zinazothaminiwa za Qatar na Misri," iliongeza.
Hamas pia ilitoa maelezo na masharti ya makubaliano yaliyofikiwa Na Israeli.
Kulingana na mpango huo Hamas inasema:
Kusitisha mapigano kwa pande zote mbili, kukomesha harakati zote za kijeshi na vikosi vya uvamizi katika maeneo yote ya Gaza, na kukomesha harakati za magari yake ya kijeshi kuingia Gaza.
Kuruhusu kuingia kwa mamia ya magari ya mizigo iliyosheheni misaada ya kibinadamu ikiwemo vifaa tiba na mafuta bila ubaguzi katika maeneo yote ya ikiwemo kaskazini na kusini mwa Gaza.
Makubaliano hayo pia, yameangazia kipengele muhimu cha kuachiwa huru kwa mateka 50 wa Israel wakiwemo wanawake na watoto, pamoja na wafugwa 150 wa Palestina waliopo katika magereza ya Israeli.
Vilevile, katika muda huo wa siku nne, Israel inatakiwa kusitisha kutumia anga ya Gaza.
Pamoja na kusimamisha matumizi yote ya anga kaskazini kwa saa 6 kila siku, kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi jioni.
Wakati wa kipindi cha makubaliano, wavamizi hao wanatakiwa kuhakikisha hawatamkata au kumshambulia mtu yeyote katika maeneo yote ya Gaza.
Kuhakikisha uhuru wa kutembea kwa watu (kutoka kaskazini hadi kusini) kando ya barabara ya Salah El Din.