Kenya kwa mara ya kwanza imewaajiri raia kuhudumu katika ofisi za idara ya polisi katika mpango mpya wa kuchanganya raia katika shughuli za jeshi la polisi.
Watu 930 waliandaliwa hafla maalum ya mapkoze katika ajira zao mpya Jumanne pili, katika makao makuu ya Idara ya Ujasusi Kenya DCI jijini Nairobi.
Naibu Mkurugenzi DCI Bw John Onyango alipongeza kundi hilo kwa kuchaguliwa miongoni mwa wengi waliotuma maombi ya nyadhifa hizo.
Wafanyakazi hao wapya wa kiraia ni miongoni mwa 930 walioajiriwa ili kuongeza rasilimali watu katika Huduma ya Kitaifa ya Polisi.
Kati yao, kuna waajiriwa wapya 203, watakaohudumu kama wahasibu, mafundi, maafisa wa usimamizi wa rekodi, wasimamizi wa ofisi, na makarani miongoni mwa taaluma zingine.
TRT Afrika