Mvua iliyoanza Oktoba nchini Kenya imeleta mafuriko katiak sehemu tofauti za nchi/.

Hali imekuwa ya utata katika sehemu za nchi ya Kenya baada ya mafuriko kuletwa na mvua iliyoanza mwezi Oktoba.

Serikali ya Kenya imesema mvua zaidi inatarajiwa kuendelea katika maeneo ya Kusini mwa nchi kati Desemba 9 na Disemba15 mwaka huu.

Hali ilivyo Nyatike katika Kaunti ya Migori nchini Kenya / Picha kutoka Kenya Red Cross

Maeneo yatakayoathiriwa na mvua hiyo ni pamoja na maeneo ya ziwa Victoria , maeneo ya milimani ya mkoa wa kati , Upande wa kaskazini mashariki mwa bonde la ufa, maeneo ya pwani na magharibi mwa Kenya.

Mvua hii inaongeza hofu ya mafuriko kuendelea.

"OperationDhibitiElnino" ambayo ndiyo jina la juhudi za serikali za kuwafikia waliaothirwa inaendelea.

Misaada inasafirishwa kwa ndege na mingine kurushwa kutoka angani katika maeneo ambayo ni ngumu kufika kwa barabara/ Picha kutoka Isaac Mwaura msemaji wa serikali 

Usafirishaji wa ndege na kurusha msaada kutoka angani unaendelea katika maeneo ambayo hayafikiki kwa barabara.

" Siku ya Alhamisi, vijiji vya Kilengwani & Mwina kata ya Tana River vilipokea tani 5 za chakula cha msaada kupitia usadizi wa kitengo cha polisi cha usafirishaji wa ndege," msemaji wa seriklai Isaac Mwaura alielezea katika ukurasa wake wa X.

Misaada mingine inapelekwa kwa boti / Picha kutoka Isaac Mwaura Msemaji wa serikali 

Mafuriko ya mto Tana utaendela kuathiri maeneo jirani na inatarajiwa kuathiri usafiri katika barabara ya Garsen hadi Lamu.

Ushirikiano unafanywa kati ya maofisa wanamaji wa serikali , na mashirika mengine binafsi kupeleka tani 8.25 ya mahitaji muhumi kupitia boti kwa vijiji vya Buyani na Marara.

Mafuriko yameuwa watu katiak sehemu tofautoi za nchi/ Picha kutoka  Kenya Red Cross

Serikali inasema watu 168 wamekufa kutokana na mafuriko hayo na idadi wa waliolazimika kuhama makwao kwa sasa ni 545,515.

TRT Afrika