Uamuzi wa Mahakama Kuu nchini kenya wa Jumatano kuhusu kesi ya mauaji imezua mjadala mpana hasa mitandaoni.
Mahakama Kuu ilimhukumu Joseph Irungu maarufu kama Jowie adhabu ya kifo baada ya kushtakiwa kumuua mfanyabishara Monica Kimani Septemba 2028.
Kesi ya mauaji ya Monica Kimani iliongelewa sana nchini Kenya baada ya Jowie kushtakiwa pamoja na alikuwa mwanahabari maarufu nchini Kenya, Jacque Maribe. Na ni yeye aliyesoma habari za mauaji hayo katika runinga ya CITIZEN TV usiku huo wa mauaji.
Hata hivyo, Mahakama Kuu ilimuondolea Maribe shtaka hilo na hatimae kumuachia huru, huku Jowie akipatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake.
" Ni uchungu mno lakini muamchie huru ... Mungu atamhukumu kulingana na makosa yake," alisema hk...hezzy, mmoja ya wachangiaji katika mtadao wa X.
"Tupinge mauaji," alisema Inheritance.
"Uamuzi huo ulikuwa mkali sana kwa vile ushahidi ulikuwa wa kimazingira kutokana na kukosa ukweli wa moja kwa moja," amesema @OsoiPatrick katika X," Jaji Nzioka alitoa hukumu kulingana na uwezo wa JOWI au kazi yake ya zamani."
Maribe aliachiliwa huru katika kesi ya mauaji ya Monica Kimani mnamo Februari 9, 2024, na Jaji Grace Nzioka wa Mahakama Kuu ya Milimani. Kulingana na Jaji Nzioka, shtaka lililoletwa dhidi ya Maribe halikuwasilishwa ipasavyo.
Wakati huo huo, Wizara ya Huduma ya Umma imekana taarifa kwamba, awali Maribe aliteuliwa kama msemaji katika Wizara hiyo.
Katika taarifa ambayo imetowela na Tume hiyo kwa vyombo vya habari siku ya Alhamisi, Tume ilikataa uteuzi huo ikisema kuwa haikuhusika katika ajira ya nafasi hiyo.
"Nafasi iliyotajwa itajazwa kupitia mchakato wa ushindani wa ajira iwapo nafasi itatokea," taarifa hiyo inayohusishwa na mwenyekiti wa Tume, Anthony Muchiri imesema.
Nini baada ya hukumu ya kifo?
Hukumu ya kifo ndiyo hukumu ya juu zaidi nchini Kenya na kwa kawaida, ina maanisha mhukumiwa anafaa kuuliwa kama adhabu inavyosema.
Hata hivyo, kulingana na sheria, bado Irungu anaweza kukataa rufaa ndani ya siku 14 tangu kutolewa kwa hukumu hiyo.
Rais ndiye peke mwenye uwezo chini ya sheria kuidhinisha kuuaawa kwa mtu aliyehukumiwa kifo. Hata hivyo tangu 1987 serikali haijaidhinisha mauaji ya mfungwa.
Wataalamu wa masuala ya sheria wanasema kwa sasa kuna mtindo duniani wa kuondoa hukumu ya kifo.
Hapo awali, ilikuwa lazima mtu anayeua apate hukumu ya kifo lakini mahakama kuu nchini Kenya iliaamua kuwa hukumu ya kifo ya lazima ni kinyume na katiba.
Kwa hivyo, sasa majaji wana uhuru wa kuamua kutoa hukumu ya kifo au la.