Madakitari wa Kenyatta National Hospital wanasema kutia damu katika mishipa ya mtoto akiwa tumboni ulichukua kati ya nusu saa na saa moja/ Picha:  Kenyatta National Hospital

Hospitali ya Kenyatta National hospital, KNH, nchini Kenya inajivunia mafanikio makubwa ya afya.

Madaktari kwa hospitali hiyo wameweza kumuongeza mtoto damu mishipani kwa mafanikio akiwa kwenye tumbo ya mama yake.

Madaktari wanne na wauguzi watatu walihusika katika matibabu hayo.

Utiaji damu katika mishipa ya mtoto akiwa ndani ya tumbo ya mama ni njia ambayo seli nyekundu za damu kutoka kwa mfadhili hudungwa ndani ya mtoto. Inaweza kupendekezwa wakati mtoto ana upungufu wa damu.

Daktari anasema kati ya mimba nne mama huyo alikuwa amefanikiwa kujifungua mtoto mmoja tu.

"Mama huyu ana mtoto mmoja tu. wengine wawili waliaga kwasababu ya changamoto za damu," dkt. Rosa Chemwey alisema.

"Tunaweka bidii kuhakikisha kuwa huyu anabaki hai na anazaliwa vizuri. Huyu mtoto ana umri ya wiki 25 na siku tatu," ameongezea.

Kuongeza damu katika mishipa ya mtoto akiwa tumboni ulichukua kati ya nusu saa na lisaa moja.

TRT Afrika