Nchini Kenya, haijulikani idadi ya watu wasio na utaifa lakini Umoja wa Mataifa unasema kuwa unakadiria takriban watu 18000 tangu kusajiliwa kwa Wamakonde mnamo 2016. Picha : Juma Masoud

Jamii ya Wapemba nchini Kenya sasa inatambulika rasmi kama mojawapo ya jamii za kikabila nchini Kenya baada ya rais kuwapa Uraia siku ya Jumamosi.

Juma Masoud, mmoja wa wanufaika wa uraia huo, alipokea hatua hiyo kwa furaha kubwa, lakini anasema ni ushindi uliosubiriwa muda mrefu tangu karne za babu yake.

'Nina furaha sana. Nimepitiwa na hisia."

Imekuwa shida kwa miaka minane, lakini ukweli ni ushindi kwa babu na bibi yangu na watu wangu ambao walihamia Kenya karibu karne mbili zilizopita,’’ anaiambia TRT Afrika.

Juma sasa anaishi na watoto wake wanane na wake wawili katika boma lao ndogo huko Mayongu, kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya.

Anasema alihofia watoto wake kuishi aina ya maisha aliyoishi alipokuwa mdogo. Anasema hakuwa hapa wala huko.

‘’Nilikuwa naishi kama mgeni nyumbani kwangu, sikukubaliwa popote. Siwezi kupata huduma.’’ Anaiambia TRT Afrika. ‘’Mambo madogo unayoyachukulia kuwa ya kawaida, kama vile kumsajili mtoto wako shuleni ilikuwa ndoto ya mbali kwa familia yangu. Nina furaha sasa naweza kutembea kama Mkenya mwingine yeyote.’’

Kisa cha Juma kinafanana na watu wengine 7000 katika jamii yake.

Kenya, nchi yenye zaidi ya watu milioni 50 inajivunia kuwa na jamii  44 zilizosajiliwa, na sasa Wapemba wanafikia 45. Picha Juma Masoud

Wanaitwa Wapemba, kama wanavyowaita waswahili watu kutoka kisiwa cha Pemba. Ingawa Pemba ni mojawapo ya visiwa vya Zanzibar ambavyo ni sehemu ya Muungano wa Tanzania, Juma hakuweza tu kufunganya familia yake na kuhamia huko.

‘’Pengine nina familia fulani huko, huwezi kujua.’’ Anaiambia TRT Afrika. ‘’ Bahati mbaya sijui mtu yeyote pale. Babu na bibi yangu walihamia Kenya miaka mingi iliyopita. Baba yangu alizaliwa nchini Kenya. Nilizaliwa nchini Kenya na familia yangu ni ya Kenya. Ni yote tunayojua.’’ Anaongeza.

Wakati wa hafla ya kumtunuku uraia Rais William Ruto alikiri kuwa jamii ya Wapemba iliteseka kwa muda mrefu bila utambulisho.

‘’Kwa miaka mingi, wao (Wapemba) wamekuwa wakiishi hapa bila uraia na kwa sababu hiyo wamepitia matatizo mengi.’’ Rais Ruto alisema kwenye hotuba yake.‘’

Kuanzia leo, Wapemba atajulikana rasmi kuwa raia wa Kenya.’’ Huku kukiwa na shangwe na shangwe, Juma na marafiki zake hawakuweza kuficha machozi yao. Utambuzi huu ni zaidi ya kitambulisho au cheti cha Kuzaliwa pekee.

‘’Hii hatimaye ina maana kuwa jamii ya Wapemba inaweza kupata huduma kamili za umma kama vile kusajiliwa shuleni, huduma za afya, hifadhi ya jamii na haki ya kufanya kazi ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikinyimwa.’’ Anasema.

Kulingana na UNHCR, kuna angalau watu milioni 10 ambao hawana utaifa duniani. Picha TRT Afrika

Mchezo wa paka na panya

‘’Nakumbuka mwaka 2007, nilikamatwa nyumbani kwangu. Polisi walinichukua kwa sababu walinipata na kitambulisho bandia.’’ Anasimulia.

‘’Nilizuiliwa kituoni kwa siku 15. Hata baada ya kuachiliwa nilitakiwa kuripoti huko mara moja kwa wiki kwa karibu miezi 6. Ilikuwa ya kufedhehesha,'' anaongeza.

Juma anasema uvamizi wa kiholela wa polisi ulimaanisha, mtu yeyote mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 alilazimika kukimbia na kujificha.

Kukamatwa mara nyingi na uonevu kutoka kwa mamlaka kulifanya maisha yao kuwa magumu.

‘’Wakati mwingine tulilazimika kutumia kitambulisho cha mtu mwingine kupata huduma fulani. Lakini hilo lilikuwa kosa na hatari kwa sababu ukibainika ungekamatwa.’’ Anakumbuka.

Kulingana na Juma, baadhi ya wanajamii waliamua kuwasajili watoto wao chini ya familia nyingine ili tu wapate nafasi ya kujiunga na shule. Sasa wanaweza kubeba kitambulisho na cheti cha kuzaliwa chenye majina yao wenyewe.

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi UNHCR Filippo Grandi alipokea habari za uraia wao akisema ‘’Laiti ningalikuwepo ili kuishukuru Kenya kwa kuchukua hatua nyingine muhimu ya kupunguza ukosefu wa utaifa.’’ Alisema katika ukurasa wake wa Twitter. ‘’Mfano mzuri kwa nchi nyingine.’’ Aliongeza.

Kulingana na UNHCR mtu asiye na utaifa ni mtu ambaye hachukuliwi kama mwananchi rasmi na serikali yoyote chini ya katiba na sheria zake.

Ina maana hana utaifa.

Baadhi ya watu huzaliwa bila utaifa huku wengine wakipoteza utaifa kutokana na matukio.

Na Umoja wa Mataifa, UN, inasema watu wengi wasio na utaifa wanaishi katika nchi walikozaliwa.

Kenya, nchi yenye zaidi ya watu milioni 50 inajivunia kuwa na jamii 44 zilizosajiliwa, na sasa Wapemba wanakuwa wa 45.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuna zaidi ya watu milioni 10 wasio na utaifa duniani huku karibu milioni 1 kati yao wakiwa barani Afrika.

Nchini Kenya, haijulikani idadi ya watu wasio na utaifa lakini Umoja wa Mataifa unasema kuwa inakadiria takriban watu 18000 tangu kusajiliwa kwa watu wa Makonde mnamo 2016.

Jamii zingine ambazo zilikubaliwa hivi majuzi kuwa raia wa Kenya ni pamoja na jamii za Wahindi na Wamakonde na baadhi ya Wasomali.

Juma anasema watu wake walipigana kwa miaka mingi, ili kutambulika. Kwa hivyo hatimaye sasa Wakenya wakiitwa, naye pia ataweza kuitika.

TRT Afrika