Milio ya risasi ilisikika karibu na kambi ya kijeshi katika kitongoji hicho. Picha: AFP

Ufyatulianaji wa risasi kati ya wanajeshi wa Ulinzi wa Taifa wa Guinea-Bissau na vikosi maalum, umesikika, kulingana na vyanzo vya kijeshi na ujasusi.

Haya yanajiri huku Rais Umaro Sissoco Embalo, aliyechaguliwa Disemba 2019, akiwa Dubai katika mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa Hali ya Hewa (COP28).

Waziri wa Fedha Souleiman Seidi na Katibu wa Hazina Antonio Monteiro waliitwa na mahakama mapema Alhamisi kabla ya kuwekwa kizuizini.

Polisi waliwahoji wakuu hao wawili kwa saa kadhaa kuhusu utoaji wa dola milioni 10 kutoka kwenye hazina ya serikali, kulingana na vyanzo ambavyo vilizungumza kwa sharti la kutotajwa kutoka na sababu za kiusalama.

Wabunge walikuwa wamemuuliza Seidi kuhusu kujiondoa wakati wa kikao Cha Bunge la Taifa Jumatatu.

Alidai kuwa uondoaji huo ulikuwa halali na ulikuwa na lengo la kusaidia sekta binafsi ya kitaifa.

Wanajeshi wa Ulinzi wa Taifa waliwapeleka Seidi na Monteiro katika eneo lisilojulikana siku ya Alhamisi usiku kabla ya kutafuta kimbilio katika kambi za kijeshi katika wilaya ya Kusini Ya Santa Luzia, vyanzo vilisema.

Vikosi maalum viliingilia kati baada ya majaribio kadhaa ya upatanishi kutofanikiwa, na utulivu ukarejea baada ya vikosi kubadilishana risasi, vyanzo vilisema.

Maafisa wa kikosi cha msaada wa utulivu cha Guinea-Bissau, kilichotumwa nchini na Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi (ECOWAS), walionekana wakishika doria mitaa ya Bissau Ijumaa asubuhi, mwandishi wa habari wa AFP aliripoti.

Uimarishaji huu wa usalama wa rais unakuja wakati ambapo mapinduzi au majaribio ya mapinduzi yanaongezeka Afrika Magharibi, hasa Gabon, Niger, Mali, Burkina Faso, Guinea na tena wiki hii, Sierra Leone.

Ris Embalo aliwateua majenerali wawili mnamo Septemba, Thomas Djassi na Horta Inta, kama mkuu wa Usalama wa Rais na Mkuu wa Wafanyakazi mtawaliwa. Ingawa nafasi hizo, zimetambulishwa katika chati rasmi ya wadhfa za serikali, hazikuwa zimejazwa kwa miongo kadhaa.

AFP