Makubaliano ya amani yalitiwa saini 2 Novemba 2022 / Picha: AFP

Makubaliano kati ya serikali ya Ethiopia na kikundi cha Tigray People's Liberation Front, TPLF mjini Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 2 Novemba mwaka 2022 ulianzisha safari ya amani nchini humo.

Eneo la kaskazini mwa Ethiopia lilikumbwa na vita kati ya serikali na kikundi hicho kuanzia tarehe 4 Novemba 2020.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitangaza vita dhidi ya kikundi hicho cha TPLF, kwa madai ya kushambulia kambi ya kijeshi yenye gala la silaha, kaskazini mwa nchi.

Vita hivyo zilizua wito kutoka jumuia ya kimataifa kutaka kusitishwa na hata kupelekea seriklai ya Marekani na Muungano wa Ulaya kuiwekea Ethiopia na watu kadhaa vikwazo kwa nia ya kukomesha vita hivyo.

Mwaka mmoja baada ya makubalioni ya amani bado wengi wanaishi katika makambi hawajaweza kurejea makwao/ picha AFP 

Baada ya makubaliano ya Pretoria ya 2021, sasa serikali na TPLF zinasema lengo lao ni kurejesha hali ya utulivu kaskazini mwa nchi hiyo.

Makubaliano ya amani yaliongozwa na Umoja wa Afrika chini ya ujumbe wa marais wa zamani Olusegun Obasanjo (Nigeria), Uhuru Kenyatta (Kenya) na makamu wa rais wa zamani Pumzile Mlambo-Ngcuka wa Afrika Kusini.

"Makabidhiano ya silaha nzito, kurejeshwa kwa huduma muhimu, kuanzishwa tena kwa shule na shughuli za kibiashara katika eneo la Tigray, kuanzishwa kwa utawala wa muda wa Tigray, ni hatua muhimu zinazonyesha dhamira ya pande zilizotia saini kupanga njia ya amani na usalama endelevu nchini Ethiopia," mwenyekiti wa tume wa Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amesema.

Hali Ikoje kaskazini mwa Ethiopia?

Mwezi Mei 2021 vita vilipoanza serikali ya Ethiopia iliorodhesha kikundi cha Tigray People's Liberation Front kama waasi.

Lakini baada ya kutia saini ya makubaliano ya amani Novemba 2022, bunge la Ethiopia mwezi Machi 2023, liliamua kuondoa jina hilo la uasi katika orodha ya kikundi vya magaidi.

" Kuna jitahada za kurejesha huduma tofauti hapa Tigray, kama benki na mawasiliano," Ato Assefa amesema.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anasema serikali yake inajitahidi kurejesha hali ya kawaida kaskazini mwa nchi/ picha: AFP 

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kuna takriban watu milioni 1.8 waliokimbia makazi yao wakati wa vita.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, linasema, takribani watu 234,000 wapo katika mji mkuu wa Tigray Mekele.

Wengi wamelazimika kuingia mitaani na kuanza kuomba, hali zao zikiwa mbaya zaidi baada ya matumizi mabaya ya shehena za misaada, hivyo kusababisha Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP na la Marekani USAID kusitisha msaada wa chakula kwa Tigray mwezi Mei.

Wakati huo huo, mfumuko wa bei umeongezeka nchini Ethiopia na watu walipoteza ajira huko Tigray. Wengi wanatatizika kununua mahitaji ya kimsingi, ikiwa ni pamoja na chakula.

Maisha ya wengi yamebaki kuwa ya sintofahamu kasakazini mwa Ethiopia / Picha: AFP

"Maeneo ambayo yalikuwa mazuri kwa ajili ya uwekezaji sasa ni makambi ya waliathiriwa na vita hivi, " anaongezea mkazi mwengine wa Tigray.

"Kuna watu wengi ambao bado wamekwama katika makambi ya wakimbizi, hawajaweza kurejea nyumbani licha ya makubaliano haya ya amani, kuna wanafunzi hawajawahi kupata nafasi ya kurejea nyumbani na shuleni pia."

Yared Berhe Gebrelibanos, ambaye anaongoza ASCOT (Muungano wa Mashirika ya Kiraia ya Tigray), anasema mapigano yameisha ingawa maisha bado ni magumu.

"Bado asilimia 90 ya wakazi wa Tigray wanategemea misaada. Na hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya," anasema na kuongeza, "Mimi ninaweza kupata akiba yangu na kupata mshahara wa kawaida lakini nina bahati. Watu wengi hawalipwi chochote."

"Inavunja moyo kushuhudia mateso mengi."

Bado mikakati ya kuwapa haki waliaothiriwa na vita hivyo haijakamilika.

Mamlaka ya Tume ya Kimataifa ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu (ICHREE) nchini Ethiopia imesimamishwa.

Tume hiyo ilianzishwa Septemba 2022 chini ya azimio lililoongozwa na Umoja wa Ulaya kwa nia ya kupepeleza ukiukwaji wa haki za binadamu katika vita vya kaskazini mwa Ethiopia.

Hata hivyo awamu yake imesimamishwa Oktoba mwaka huu,

TRT Afrika