Kulingana na makadirio mapya ya Usalama wa Chakula yaliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), watu milioni 17.7 kote nchini Sudan, wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula.
"Idadi kubwa ya watu walio na uhaba mkubwa wa chakula wako katika majimbo yaliyoathiriwa na viwango vya juu vya vurugu, ikiwa ni pamoja na Darfur Kuu, Greater Kordofan na Khartoum - hasa katika eneo la miji mitatu la Khartoum, Bahri na Omdurman," taarifa ya UN FAO imesema.
Vita nchini humo vilianza tarehe 15 mwezi Aprili kata ya jeshi la Sudan na kikundi cha Rapid Support Forces.
Jambo linalochangiwa zaidi ni hili la uzalishaji mdogo wa kilimo, bei ya juu ya chakula, majanga ya hali ya hewa na watu kuhama makazi yao kulingana na wataalamu.
Ghasia zilizoenea zimesababisha zaidi ya watu milioni sita kuyahama makazi yao, wakiwemo zaidi ya milioni tano ambao ni wakimbizi wa ndani na zaidi ya milioni moja waliotafuta hifadhi katika nchi jirani.
Idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani wanatoka maeneno nane, huku jiji la Khartoum likiwakilisha sehemu kubwa zaidi ya asilimia 67.
Idadi ya watu waliokimbia makazi yao wametawanyika katika majimbo yote 18 ya Sudan na kuenea nje ya mipaka ya nchi hiyo, hasa Chad, Sudan Kusini na Misri.