Idara ya u[elelezi Kenya inasema watu wnengi mno wanapotosha kupitia mitandao | Picha: Getty

Shirika hilo kwa jina 'Open Observatory of Network Interference (OONI), limesema kuwa upatikanaji wa mitandao ya kijamii nchini humo umejiri bila usumbufu baada ya serikali ya Ethiopia kuondoa vizuizi vya mitandao kwenye mitandao mikuu ya kijamii baada ya kufungwa mapema Februari na kuzuia upatikanaji.

Wadau mbalimbali wakiwemo Baraza la Vyombo vya Habari la Ethiopia pia yaliishauri serikali kuondoa vikwazo hivyo na kurejesha huduma za mtandao katika sehemu za nchi.

Wakati wa vizuizi hivyo, Waethiopia waliamua kutumia VPN kufikia mtandao na mitandao ya kijamii.

Mwezi uliopita wa Juni, mkurugenzi Mtendaji wa Ethio-Telecom, yenye wateja wa intaneti milioni 33.9 Frehiwot Tamiru, aliliambia Bunge kwamba vikwazo vya mitandao ya kijamii vilipelekea "uzoefu wa kukatisha tamaa" kwa wateja na kwamba kampuni itafanya kazi kutatua suala hilo, ingawa alisema uamuzi huo ulikuwa nje ya uwezo wake.

TRT Afrika