Uwanja huo wa ndege utachorewa sanifu ya ujenzi wake na kampuni ya Uhandisi ya Sidara iliyoko Dubai /Picha: Reuters 

Ethiopia imetia saini makubaliano ya usanifu wa uwanja mpya wa ndege wa njia nne ambao utakuwa mkubwa zaidi barani Afrika ujenzi utakapokamilika mnamo 2029, mkuu wa shirika la ndege la Ethiopian Airlines linalomilikiwa na serikali alisema Ijumaa.

Kikiwa karibu na mji wa Bishoftu, karibu kilomita 45 (maili 28) kutoka mji mkuu Addis Ababa, uwanja huo wa ndege utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 100 kwa mwaka na kutoa maegesho ya ndege 270, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Ethiopia Mesfin Tasew aliambia mkutano wa waandishi wa habari.

''Kampuni ya uhandisi na ushauri yenye makao yake makuu Dubai ya Sidara itasanifu uwanja wa ndege,'' mkurugenzi wa uendeshaji wa kampuni hiyo Tariq Al Qanni alisema.

Mipango ya kujenga uwanja wa ndege ilitangazwa kwa mara ya kwanza mnamo 2018.

Mesfin alisema Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Addis Ababa, kitovu kikuu cha sasa cha shirika kubwa la ndege barani Afrika, hivi karibuni utafikia uwezo wake wa kuhudumia abiria milioni 25 kwa mwaka.

"Ni mradi wa miaka mitano (ambao) utakamilika mwaka wa 2029. Utakuwa mkubwa zaidi barani Afrika," Mesfin alisema.

Reuters