Waziri wa Uchukuzi wa Ethiopia amewasilisha ripoti yake ya miezi sita kwa Baraza la Wawakilishi, akielezea nia ya nchi hiyo kupiga marufuku kuingiza magari yanayotumia mafuta.
Kwa sasa, Ethiopia itakuwa tayari kupokea magari yanayotumia nishati ya umeme kwa matumizi binafsi, kulingana na Alemu Sime.
Sime amesema uamuzi huo utatakelezwa kikamilifu na serikali ya nchi hiyo.
Uamuzi huu ni mpango mkakati wa Ethiopia katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuongezeka kwa gharama zinazohusisha matumizi makubwa ya mafuta.
Mwaka 2023, Ethiopia iliondoa kodi nyingi za uagizaji bidhaa ili kuongeza hamasa ya kununua magari na kuanzisha mitambo ndani ya nchi hiyo.
Kwa sasa, nchi hiyo kutoka pembe ya Afrika inakadiriwa kuwa na magari yanayotumia nishati ya umeme 7,200 kati ya 1.2 milioni yanayopatikana nchini humo, huku mji mkuu wa Addis Ababa ukiwa na vituo vitatu tu vya kujazia nishati.