Waziri Mkuu wa Ethioipia Abiy Ahmed amemteuwa Gedion Timotheos aliyekuwa Waziri wa Sheria kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.
Gedion Timotheos ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Taye Atske-Selassie, ambaye aliteuliwa kuwa Rais wa nchi hiyo hivi karibuni.
Vyombo vya habari vya serikali vinaripoti kwamba Waziri Mkuu Abiy Ahmed pia alitangaza uteuzi wa baraza la mawaziri.
Salamawit Kassa, ambaye hapo awali aliwahi kuwa Waziri wa nchi wa Huduma ya Mawasiliano ya Shirikisho, ameteuliwa kuwa Waziri wa Utalii.
Hanna Arayaselassie anachukua jukumu la Waziri wa Sheria baada ya kuwa Kamishna wa Tume ya Uwekezaji ya Ethiopia (EIC).
TRT Afrika