Serikali ya Ethiopia siku ya Ijumaa ilitangaza hali ya hatari katika eneo la Amhara. kufuatia siku kadhaa za mapigano kati ya wanajeshi na wanamgambo wa eneo la hilo wanaoitwa Fano.
Eneo la Amhara ndilo eneo la pili kwa ukubwa nchini Ethiopia.
Mapigano yaliyozuka mapema wiki hii yamekuwa tishio kwa usalama .
Baraza la mawaziri lilisema kuwa hali ya hatari imekuwa muhimu kwa ajili ya kudhibiti mzozo ulioletwa na makundi ya silaha , ili kuhakikisha amani na usalama katika eneo hilo.
Baraza lilibaini kuwa serikali imekuwa ikitoa wito kwa vikundi vyenye silaha katika mkoa huo kufuata njia ya kisheria na amani.
Serikali ya mkoa wa Amhara mnamo Alhamisi iliomba usaidizi wa ziada kutoka kwa serikali kuu ili kurudisha hali ya utulivu.
Wanamgambo hao wamekuwa tishio kwa shughuli za kisiasa, kijamii na kiuchumi katika eneo hilo, kulingana na baraza hilo.
Mapigano yaliyozuka mapema wiki hii yamekuwa mgogoro mkubwa zaidi wa usalama nchini Ethiopia tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili katika eneo jirani la Tigray kumalizika Novemba mwaka jana.
Halmashauri ya mkoa wa Amhara Alhamisi iliomba usaidizi wa ziada kutoka serikali kuu ili kuthibiti mashambulizi ya vikundi vya silaha.