Bunge la Ethiopia limeidhinisha muswada wa kurejesha mali na kuwa sheria.
Muswada huo uliwasilishwa kwa wabunge mnamo Juni 2024, ukapelekwa katika Kamati ya Kudumu ya Sheria na Haki kwa uchunguzi zaidi.
Tangazo hilo, lililoidhinishwa Januari 9, 2025, linalenga kuipa serikali mamlaka ya kukamata mali iliyopatikana kupitia mapato ambayo hayajawekwa wazi.
"Lengo la msingi la sheria hii ni kuweka mifumo kamili ya kisheria ya kurejesha mali inayohusiana na uhalifu wote wote unaoleta mapato," lilisema tangazo hilo.
Sheria mpya, ambayo inalenga mali inayoonekana na isiyoonekana inajumuisha wigo mpana wa mali, ikiwa ni pamoja na mikopo ya benki, hisa, bondi na hisa nyengine zenye manufaa ya kiuchumi.
Chini ya sheria hii, mali zinazopatikana kupitia njia ambazo hazijafichuliwa zitachukuliwa kwa kukiuka sheria ya uhalifu na ufisadi.
Tangazo hilo linasema kwamba "madai ya kurejesha mali ambayo haijaelezewa yanaweza kuwasilishwa kortini" kwa mali iliyopatikana ndani ya miaka kumi iliyotangulia, ikiwa thamani ya mradi ambayo haijaelezewa itazidi dola 79,491.