Katika kikao maaluam Ijumaa, bunge la Ethiopia llimeamua kuongeza muda wa hali ya hatari kwa miezi sita zaide katika katika eneo lake la Amhara, kaskazini mwa nchi.
Watu wa Amhara ndiyo wenye idadi ya pili kubwa zaidi nchini humo baada ya kabila la Oromo.
Uamuzi huo unakuja wakati eneo hilo likiendelea kukabiliwa na mzozo wa kijeshi unaohusisha vikosi vya serikali ya ulinzi kwa upande mmoja na wanamgambo wa Fano kwa upande mwingine.
Pendekezo la kuongea wa muda wa hatari liliwasilishwa na Waziri wa Sheria, Gedion Timothios, ambaye alisisitiza ulazima wa kuongezwa muda wakati mkutano huo.
Bunge limesema kuongeza muda huo una nia ya kudumisha "amani na usalama wa watu" huku kukiwa na mzozo wa kijeshi unaoendelea katika eneo zima.
Serikali ilitangaza kuanzishwa kwa hali ya hatari ya miezi sita mnamo Agosti 2023, na kuihalalisha kama muhimu kwa kulinda amani na usalama wa umma na kutekeleza sheria na utulivu.
Mzozo Amhara ulianzaje?
Waziri Mkuu Abiy Ahmed alisifu kikundi hicho cha Fano, pamoja na kikundi cha wapiganaji wa kutoka kabila la Oromo linaloitwa Qerro, kwa jukumu lao katika mabadiliko ya kisiasa yalifanyika na kumweka usukani mwaka 2018.
Wapiganaji hao wa Amhara walipigana pamoja na wanajeshi wa serikali wakiiunga mkono jeshi hilo katika vita vya kati ya serikali na eneo la kaskazini mwa nchi Tigray. Hii ilikuwa kati ya mwaka 2020 na 2022.
Hata hivyo ushirikiano huo muungano huo ulivunjika wakati serikali ya Abiy Ahmed na viongozi wa Tigray walifikia makubaliano mwaka 2022, ambayo yalimaliza mzozo huo.
Wakati Waziri Mkuu Abiy Ahmed alipohamia kudhibiti sasa wanamgambo wa Amhara, uhusiano ulizidi kuwa mbaya.