Ethiopian Airline

Ethiopia imeondoa marufuku ya kusafiri kwa miaka 30 kwa zaidi ya raia 10,000 ambao hapo awali walikuwa wamezuiwa kusafiri nje ya nchi.

Zaidi ya raia 10,000 wa Ethiopia ambao walizuiwa kuondoka nchini tangu 1994 sasa wanaweza kusafiri kwa uhuru.

Serikali ilisema iliwapiga marufuku kwa sababu ya usalama na maslahi ya kitaifa.

Mabadiliko haya muhimu yalitangazwa na Selamawit Dawit, Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Uhamiaji na Uraia, wakati wa mkutano na waandishi wa habari wiki iliyopita.

Selamawit alifichua kwamba watu hawa walikuwa wamepigwa marufuku kusafiri kimataifa tangu 1994.

Zaidi ya hayo, aliripoti kwamba ofisi yake ilitoa hati za kusafiria milioni 1.1 katika mwaka wa fedha uliomalizika hivi karibuni.

Ripoti zinaonyesha kuwa kumekuwa na zaidi ya maombi 350,000 ya hati za kusafiria yanayosubiri.

Katika kipindi hicho, hatua za kisheria zilichukuliwa dhidi ya wageni 18,000 wanaoishi Ethiopia na hati zisizo halali, na kusababisha kufukuzwa kwa watu 6,000.

Kurugenzi ya Huduma ya Uhamiaji na Uraia pia imesema ilichukua hatua kwa wahamiaji 18,000 ambao walikuwa wakiishi nchini bila hati halali.

Baadhi waliripotiwa kughushi nyaraka.

Wengine walitegemea hati zilizoisha muda wake. Kati ya hao, takriban 6,000 waliripotiwa kufukuzwa katika nchi yao ya asili. Hata hivyo, ofisi hiyo haikutaja nchi wanazotoka.

TRT Afrika