Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amefanya uteuzi wa kihistoria kwa kumtaja Teyiba Hassen kuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa kike kuongoza idara ya Huduma ya Wakimbizi na Waliorejea nchini humo, maarufu (RRS).
Pembe ya Afrika, eneo lenye hali tete kutokana na changamoto za uhamiaji, litakuwa mojawapo ya majukumu ya Teyiba kwani anatarajiwa kusimamia vikamilifu kutatua changamoto za wakimbizi nchini humo.
Wengi wa wakimbizi hao wanatafuta hifadhi kufuatia upungufu wa misaada ya kibinadamu na maendeleo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, wafadhili na washirika.
Teyiba mwenye uzoefu wa kufanya kazi katika mazingira magumu, ikiwemo kuongoza operesheni ya wakimbizi nchini Ethiopia, ana jukumu la kuzidisha juhudi za kusimamia mwitikio tata wa wakimbizi nchini Ethiopia, inayo walau zaidi ya wakimbizi milioni moja.
Pembe ya Afrika, eneo lenye hali tete, litakuwa mojawapo ya majukumu ya Teyiba ambaye pia ni mshauri wa masuala ya Kijamii wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed. Teyiba pia ametangazwa pia kuwa Meya wa mji wa Shashemene na Naibu Rais wa jimbo la Oromia.