Ethiopia inasema  zaidi ya miche bilioni 2 ya kahawa, zaidi ya nusu bilioni ya miche ya matunda na zaidi ya mimea milioni 400 ya chai iko kwenye maandalizi/ picha kutoka Waziri Mkuu Abiy Ahmed 

Ethiopia inalenga kuongeza mazao yake ya kahawa na chai kwa kutayarisha miche zaidi ya kupanda mwaka huu.

" Katika mwaka uliopita, zaidi ya miche bilioni 2 ya kahawa, zaidi ya nusu bilioni ya miche ya matunda na zaidi ya mimea milioni 400 ya chai iko kwenye maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa upanzi kwa kuzingatia kuboreshwa," waziri mkuu Abiy Ahmed amesema,

" Tukiweza kupanda miche hii na kuikuza kwa uzalishaji, itakuwa na athari kubwa kwa uchumi wetu kwa ujumla na juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,: Ahmed ameongezea katika akaunti yake ya X.

Ni zaidi ya miaka mitano sasa tangu serikali ya Ethiopia ianze upanzi mkubwa wa miche nchi nzima kupitia mpango wake wa 'Urithi wa Kijani' ulioanzishwa na Waziri Mkuu.

Mradi huo wa kurejesha kijani aina tofauti nchini ulionza mwaka 2019 na kukamilika 2023.

Serikali hiyo sasa inasema imepanda zaidi ya miche bilioni 32.5 ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na matunda ya aina mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mpango huo.

Ethiopia inatekeleza mpango huu mkuu kwa lengo la kusaidia juhudi zinazoendelea za taifa za kuongeza tija ya kilimo na kuhakikisha kujitosheleza kwa chakula kwa kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Waziri mkuu Abiy Ahmed alianzisha mradi wa kitaifa wa kupanda miti mwaka 2019/ picha kutoka Ofisi ya Waziri mkuu Ethiopia  

Licha ya changamoto za kisiasa, vifaa na hali ya hewa zinazoathiri sekta ya kahawa ya Ethiopia katika miaka ya hivi karibuni, kahawa inasalia kuwa chanzo kikuu cha mapato ya nje ya nchi, na kuzalisha takriban 30-35% ya hisa nzima ya nchi.

Juhudi za kuimarisha hali mzuri ya hewa kwa lishe bora imepewa msukumo na ufadhili moya kutoka kwa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), na Serikali ya Ethiopia imeanza rasmi mpango wa muda mrefu wa kukabiliana na ukataji miti na kuboresha sekta ya kahawa.

Mpango huo ni wa dola milioni 20.8.

Mradi huo unaitwa "Kuzuia Upotevu wa Misitu, Kukuza Urejeshaji, na Kuunganisha Uendelevu katika Minyororo ya Thamani ya Kahawa ya Ethiopia na Mifumo ya Chakula."

Umeundwa kuzuia ukataji miti, kukuza upandaji miti na kutoa msaada wa soko kwa wazalishaji wa kahawa wa Ethiopia.

Serikali hiyo imesema chini ya mradi huu itspitisha rasmi sera mpya jumuishi ya matumizi ya ardhi huku ikitafuta kuboresha maisha ya takriban watu 440,000.

Mradi huo unalenga kurejesha hekta 10,500 za ardhi ya kahawa isiyo na tija, huku ukirejesha na kusimamia hekta 60,000 za ardhi muhimu ya misitu.

TRT Afrika