Muswada mpya wa nyumba nchini Ethiopia unalenga kuongeza uwajibikaji miongoni mwa wajenzi na wauzaji wa nyumba/ Picha: Almashauri ya jiji la Addis Ababa

Muswada mpya upo mbele ya Bunge la Ethiopia ukilenga kutoa sheria mpya katika sekta ya nyumba.

Muswada huo, unaolenga kuongeza uwajibikaji miongoni mwa wajenzi na wauzaji wa nyumba na kulinda maslahi ya wanunuzi, ilijadiliwa na baadaye kupelekwa kwenye Kamati ya Kudumu ya Miji na Uchukuzi kwa ukaguzi zaidi.

Muswada huo kwa mfano, unatanguliza ulinzi kwa wanunuzi, kama vile kuwataka wajenzi na wauzaji kutoa maelezo ya kina ya mradi.

Wakili wa biashara Haile Bayisa alielezea mabadiliko hayo kuwa yamepitwa na wakati, akisema, "Pengo katika soko la nyumba limehitaji kuzingatiwa kwa miaka."

Kwa wanunuzi kama Temesgen Asfaw mkazi wa Addis Abeba, mageuzi yanatoa "uwazi zaidi na usalama" katika shughuli za malipo.

Rasimu hiyo pia inajumuisha mahitaji kuwa mjenzi lazima awe na kuanzia nyumba 50 ili apate leseni. Pia atahitajika kukamisliha ujenzi kwa angalau asilimia 80 kabla ya kuuza.

Ingawa wengine wanaona hatua hizi ni muhimu ili kuongeza viwango, wengine wanahoji kuwa inaweza kuzuia miradi midogo ambayo bado inaweza kutekelezwa kisheria.

Sekta ya nyumba Ethiopia imekuwa kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni, huku wajenzi wakijitahidi kukidhi mahitaji ya nyumba yanayoongezeka katika miji kama Addis Ababa.

Sekta hiyo pia imekabiliwa na masuala ya miradi iliyocheleweshwa na ahadi ambazo hazijatimizwa, na kusababisha mmomonyoko wa uaminifu.

Ili kutatua matatizo haya, Bunge hivi karibuni liliwasilisha rasimu ya mswada huo unaolenga kuboresha uwazi na uwajibikaji katika soko hilo.

TRT Afrika