Demeke Mekonnen, amekuwa naibu Waziri Mkuu wa muda mrefu wa Ethiopia, na pia Waziri wa Mambo ya Nje tangu Novemba 2020/ Picha AFP

Temesgen Tiruneh, Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi na Usalama (NISS) amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Demeke Mekonnen.

Mekonnen, aliyehudumu pia kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, tangu Novemba 2020, ameondoka katika nyadhifa zote mbili mapema leo.

Hayo yamewekwa wazi katika kikao cha Wajumbe wa Kamati Kuu ya chama tawala cha Prosperity Party.

Maamuzi hayo pia yamemfanya Demeke apoteze nyadhifa zingine kwenye chama hicho, ikiwemo ya umakamu Rais wa Prosperity Party akiwakilisha mrengo wa Amhara.

Akiwa kama naibu Waziri Mkuu tangu mwaka 2012, Demeke alishika wadhifa wa Uwaziri wa mambo ya Nje wakati wa mabadiliko yaliyofanywa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed kufuatia vita katika eneo la Tigray mnamo Novemba 2020.

Hata hivyo, sababu za kuondoka kwenye nafasi hizo nyeti bado hazijawekwa wazi.

TRT Afrika