Ujenzi wa bwawa kubwa la dola bilioni 4.2 nchini Ethiopia ulianza mnamo 2011. / Picha: AFP 

Waziri Mkuu Abiy Ahmed ametangaza kuwa Ethiopia imekamilisha kujaza Bwawa lake la Grand Renaissance kwenye Mto Nile, chanzo cha mvutano wa kikanda na Misri na Sudan.

"Ni furaha kubwa kwamba ninatangaza kukamilika kwa mafanikio kwa ujazo wa nne na wa mwisho wa Bwawa la Renaissance," Abiy alisema Jumapili katika ujumbe kwenye X, zamani Twitter, ambao unakuja wakati mazungumzo kati ya nchi hizo tatu yakirejea Agosti 27.

"Kulikuwa na changamoto nyingi, mara nyingi tuliburuzwa kurudi nyuma. Tulikuwa na changamoto ya ndani na shinikizo la nje. Tumefikia (hatua hii) kwa kukabiliana na Mungu," alisema.

Waziri Mkyuu Abiy aliwapongeza raia wa Ethiopia na kuwashukuru kwa uvumilivu wao ambao alisema kuwa umefanikiwa kuzaa matunda.

“Naamini tutamaliza tulichopanga baadaye,” alisema.

Mzozo wa kikanda

Kwa makadirio ya uwezo wa zaidi ya megawati 6,000, Ethiopia inaona GERD kama kitovu cha azma yake ya kuwa muuzaji mkubwa wa umeme barani Afrika.

Huku likichukuliwa kuwa muhimu na Addis Ababa, bwawa hilo kubwa lenye thamani ya dola bilioni 4.2 limekuwa kitovu cha mzozo wa kikanda tangu Ethiopia ilipojikita katika mradi huo mwaka 2011, huku Misri ikihofia kupunguza sehemu yake ya maji ya Mto Nile.

Mazungumzo ya sasa, ambayo yalianza tena baada ya karibu miaka miwili na nusu, yanalenga kufikia makubaliano ambayo "yanazingatia maslahi na wasiwasi wa nchi hizo tatu," waziri wa umwagiliaji wa Misri Hani Sewilam alisema, akihimiza "kukomeshwa kwa hatua za upande mmoja."

TRT Afrika na mashirika ya habari