Baadhi ya magari yanayotumia umeme yakiuzwa jijini Addis Ababa, Ethiopia. /Picha: AP

Mapema mwezi huu, serikali ya Ethiopia ilipandisha bei ya mafuta kwa kiwango cha asilimia 8, kama sehemu ya mpango wa kumaliza hatua kwa hatua ruzuku zote za mafuta katika nchi hiyo ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Mamlaka imedai kufanikiwa kwa kiasi fulani katika kutekeleza marufuku ya magari yasiyo ya umeme kuingia Ethiopia, na zaidi ya magari 100,000 yanayotumia umeme sasa yanaingizwa nchini kila mwezi.

Lengo rasmi ni kuongeza idadi ya uagizaji wa kila mwezi hadi 500,000 ifikapo mwaka 2030.

Kufikia wakati huo, bwawa jipya la Ethiopia ambalo limejengwa kwenye Mto Nile linatarajiwa kuwa likizalisha nishati kwa uwezo kamili.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, katika hotuba ya televisheni mapema mwaka huu, alisema Bwawa la ''Grand Renaissance'' litaanza kuzalisha zaidi ya megawati 5,000 za nishati ya umeme ndani ya mwaka mmoja. Mamlaka imesema uwezo kama huo ungesaidia katika uhamiaji wa kutumia magari ya umeme.

Waziri wa Uchukuzi wa Ethiopia, Bareo Hassen Bareo, amesema anaamini kuwa nchi hiyo inaweza kuwa taifa lenye kupigiwa mfano katika sekta ya uchumi wa kijani, huku magari ya umeme yakipewa kipaumbele.

Serikali itawekeza katika vituo vya kuchaji vya umma, aliiambia ''The Associated Press'', na kuna mipango ya kuunda kiwanda cha kutengeneza betri za magari ya umeme ndani ya nchi ili kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje.

Hata hivyo, huko Addis Ababa, jiji la zaidi ya watu milioni 5, wana shaka kuwa nchi hiyo inaweza kufikia malengo yake makubwa ya magari ya umeme bila miundombinu na huduma zinazohitajika.

Wamiliki wachache wa gereji ambao wanaweza kurekebisha magari ya umeme yaliyoharibika wanasema wamezidiwa, huku wateja wakisema wanatozwa bei ya juu unaosababishwa na ukosefu wa ushindani katika biashara hiyo.

"Kuna gereji mbili au tatu ambazo zinaweza kurekebisha magari mapya yanayotumia nishati nchini Ethiopia na watumiaji wengi hawana uelewa wa jinsi ya kutunza magari hayo," alisema Yonas Tadelle, fundi mekanika mjini Addis Ababa.

"Kama mekanika, pia tunakosa zana, vipuri na ujuzi wa kurekebisha magari kama hayo."

Magari ya umeme mengi sasa yameegeshwa kwenye gereji na sehemu za kuegesha zikingoja vipuri zinazotarajiwa kutoka China.

Vilevile watumiaji walalamika kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo usambazaji duni wa umeme huko Addis Ababa, na uhaba wa vipori, unaotokana na bei ghali ya vipori vinayoagizwa kutoka China.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

AP